ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 12, 2009

MASHINDANO YA BALIMI MBIO ZA MITUMBWI 2009 YALIVYOFANA NDANI YA ZIWA VICTORIA.



TIMU YA TBL MWANZA IKISHEREHEKEA YALIYOKUWA YAKIJIRI LEO ENEO LA MWALONI JIJINI MWANZA. KAKA ASHRAF PLIZZZ NITUMIE MAJINA YA WADAU.


MKUU WA MKOA WA MWANZA MH.ABASS KANDORO AKIFUATILIA KWA MAKINI MASHINDANO.


WADAU WA TBL NAO KATIKA KUPIGA MAKASIA SI MCHEZO


KINYWAJI CHAO CHA KUTOSHA PEMBENI KISHA MWENDO MDUNDO MAMBO YA BALIMI NA WADAU WA TANZANIA BREWERIES WALIKUWA NA MZUKA HAO


MH. MKUU WA MKOA AKIENDESHA ZOEZI LA MAKAPTENI WA BOTI KUCHAGUA MITUMBWI AMBAPO KILA KAPTENI JINA LAKE LILISOMWA NAYE KUCHAGUA MOJA YA VIKARATASI VILIVYOFUNGWA VYENYE NAMBA ZA BOTI KWAAJILI YA MASHINDANO.


MAKAPTENI WA MITUMBWI KUMI NA MOJA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA.


MASHINDANO YALIZINGATIA SHERIA ZOTE ZA USALAMA MAJINI.


WASHIRIKI UPANDE WA WANAWAKE WALEEEE WAJA.


WA KWANZA UPANDE WA WANAWAKE NI UKEREWE.


NAFASI YA PILI WANAWAKE ILIKWENDA MWANZA.


NAFASI YA TATU WANAWAKE ILIKWENDA BUKOBA.


MUSOMA NAFASI YA NNE, YA TANO BUKOBA, YA SITA MWANZA,YA SABA NA YA NANE KIGOMA, YATISA BUKOBA NA YA KUMI IKAENDA KWA WASHIRIKI TOKA MWANZA.


WASHIRIKI WAKITAFAKARI BAADA YA SHINDANO.


WATU WALIITIKA UMATI WENYEWE UNAZUNGUMZA.


CHEKSHIA MWANAWANE.


NANI KAONAAA? ALIYEKETI NI INJINIA WA TBL MR. MKUMBO AKIFUATILIA KWA UMAKINI YALIYOMO SHUGHULINI, PEMBENI WA KATIKATI JAMES TOKA TBL NA ANAYE ONGOZA MTAMBO DJ MKALI KATIKA GAME NA UFANIKISHAJI DJ OMMY JR.


KILAKITU KILIKUWA NA MVUTO HIVYO HATA WADAU WENYEWE KUSHANGAA RUKSAAAA!


NI SEHEMU TU YA UMATI WALIOJITOKEZA ENEO LA MWALONI MAHALA MASHINDANO YALIPOFANYIKA.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Huwa nafurahia mashindano kama haya.
    Haya ni mashindano ambayo yanashindaniwa hata kwenye Olimpiki na ni michuano ambayo watu wengi wanaimudu nyumbani bila hata msaada wa serikali na wafadhili. Lakini serikali imewekeza kunakohitaji nguvu na kusiko na uwezekano wa kufanya vema.
    Ni wakati wa kuwekeza kule tunakoweza kushinda. Kama kwenye ndondi, riadha, mbio za mitumbwi, na mashindano mengine badala ya kumwaga mamilioni kwenye uwanja wa taifa unaolea wachezaji waliotelekezwa utotoni.
    Hatutasonga kama tunafunga michezo ya utoto na kutegemea kufanya vema ukubwani. Naandika kuhusu TANZANIA YANGU.... INAYOZIMA MOTO KWA PETROLI nikihusisha mambo kama haya ya kusema unataka maendeleo huku ukiyanfungia njia.
    Lakini kwa sasa labda nikuunganishe na haya niliyozungumza kuhusu kupuuza tuwezayo katika http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/08/tanzania-yanguinauza-baiskeli-na.html
    Blessings

    ReplyDelete
  2. wakuu wakiweka nguvu kidogo tu ktk mchezo huu unaweza kuvutia watalii kibao. wazungu wengi wanapenda vitu vya asili na funny esp in Africa, wengi watapenda kuja kurelax na kupiga kasia hasa huku kwao muda mrefu ni winter- snow (baridi)ndio maana hutafuta sehemu za kuota jua. I hope Mwanza ipo karibu na serengeti so it can be a good stop over ever in east Africa. it's just ubunifu tu na kuboresha mahoteli. That's all.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.