
Yanga SC leo Mei 9, 2026 inatarajiwa kushuka dimbani kuikaribisha Coastal Union katika mchezo wa kusisimua wa NBC Premier League utakaopigwa majira ya saa 12:15 jioni kwenye KMC Complex.
Kuelekea mchezo huo, benchi la ufundi la Yanga SC limeweka wazi kuwa mashabiki wanapaswa kutarajia soka la kuvutia lenye ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
Wananchi wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na morali kubwa baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo uliopita, bao pekee likifungwa na Allen Okello dakika ya 65.
Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Ahamid Moallin amesema kikosi chake kinaiheshimu Coastal Union lakini hakitabadilisha falsafa yake ya kucheza soka la kumiliki mpira na kulitawala dimba.
“Kitu ninachoweza kuwaahidi mashabiki wa Yanga ni mchezo mzuri. Sisi kama Yanga tuna namna yetu ya kucheza, msingi wetu ni kumiliki mchezo. Tunaiheshimu Coastal Union lakini hatuwezi kuacha utamaduni wetu.
Tunataka kumiliki mchezo kwa dakika zote 90, si kwa vipindi fulani. Kila mchezaji anapaswa kutoa kiwango chake cha juu kuhakikisha tunatawala mchezo na kupata matokeo mazuri,” amesema Moallin.
Kwa sasa Yanga SC inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 21, huku Coastal Union ikishika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 22, hali inayoufanya mchezo huo kuwa na presha tofauti kwa kila upande.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment