Na Victor Masangu, Kibaha
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha katika kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta chachu ya maendeleo imeamua kutumia fursa ya makusanyo ya fedha za mapato yake ya ndani katika kuhakikisha inakabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ikiwemo suala la kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa zilizopo katika kata zote 14.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr. Nicas Mawazo wakati wa kikao cha kikanuni cha baraza la madiwani robo ya tatu ya kuanzia mwezi januari mwaka huu wa 2026 hadi kufikia Machi ambapo amebaini lengo kubwa ni kuhakikisha wanawaletea mabadiliko chanya ya kimaenndeleo katika nyanja mbali mbali kupitia mapato ya ndani.
Mstahiki Meya amebainisha kwamba katika kikao hicho wamemeweza kupata fursa ya kupokea taarifa mbali mbali kutoka katika baadhi ya taasisi ikiwemo Dawasa, Tanesco, Bima ya afya, Tarura, pamoja na nyinginezo kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ambayo yataweza kuletaa tija zaidi katika kutatua changamoto mbali mbali za wananchi katika maeneo ambayo wanaishi.
"Tumefanya kikao chetu cha kikanuni cha baraza letu la madiwani na kwamba tumejadili mambo mbali mbali ikiwemo suala la upatikanaj wa huduma ya maji safi na salama, kuboresha miooundombinu ya barabara za mitaa ambapo tumeweza kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila mtaa na hii itaweza kusaidia kwa kiais kikubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara sekta ya elimu na afya ,"amebainisha Dr. Nicas
Kwa upande Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt. Rogers Shemwelekwa amesema kwamba lengo kubwa niu kuzidi kuendelea kuongeza kasi zaidi katika suala zima ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo pia yataweza kusaidia katika kutekeleza baadhi ya miradi mbali mbali ya maendeleo.
Shemwelekwa ameahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi pamoja na madiwani kwa lengo la kuweza kuleta dhana pana ya ushirikishwaji ambayo itaweza kuleta matokeo chanya kataika suala zima la maendeleo.
Nao baadhi ya madiwani wa viti maalumu akiwemo Selina Wilson katika kupambana naa maambukizi mapya ya virusi vya ukimvi (VVU) hakusita kuwahimiza wakinababa kutumia kinga kwa lengo la kuweza kuepukana na maambukizi mapya na kwamba ni vema sasa kuwahimiza umuhimu wa kutumia kondomu katika tendo la ndoa na kuacha na ngono zembe.
Naye Diwani wa viti maalumu Shufaa Mshana pamoja na Sara Uledi wamesema wameomba juhudi za makusudi zifanyika katika kuboresha sekta ya afya hasa kwa upande wa wakinamama wajawazito ambao wamekuwa wakitembea umbari mrefu katika baadhi ya maeneo kwa ajili ya kwenda kupata huduma ya kujifungua.
Kikao cha kikanuni cha baraza la madiwani robo ya tatu ya kuanzia Januari hadi machi mwaka huu kimeweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu ya barabara za mitaa, kuboresha huduma ya maji safi na salama, upatikanaji wa bima ya afya kwa wote, suala la afya, elimu pamoja na mambo mengine yaa msingi kwa ajili ya maslahi ya wananchi kwa ujumla.
Tupe maoni yako



0 comments:
Post a Comment