ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 9, 2026

SIMBA SC NAYO YACHANGIA MAPATO KWA TRA UNITED ARUSHA, ZATOKA SULUHU

 


TIMU ya Simba SC imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. 

Kwa matokeo hayo, TRA inayofundishwa na Kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba ikiizidi tu wastani wa mabao Dodoma Joni FC baada ya wote kucheza mechi 18. 

Kwa upande wao Simba SC wanafikisha pointi 36 katika mchezo wa 17, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Yanga ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment