NA ALBERT G.SENGO/FELA/MISUNGWI/MWANZA
Tahadhari imetolewa na Wataalamu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) katika mkutano wa hadhara wa kutoa elimu ya usalama kwa wakazi wa Kijiji cha Fela wilayani Misungwi, ambako mradi huo wa kimkakati unatekelezwa na serikali. Afisa Usalama Mahali Pa Kazi wa TRC Richard Msungu amesema lengo la shirika hilo kutoa elimu ya usalama kwa wananchi wanaoishi katika ushoroba wa reli ya SGR ni kuona wanakuwa salama ikiwa watazingatia alama za usalama kwa kutumia vivuko sahihi vya kuvukia binadamu, wanyama na magari. Kwa mujibu wa mhandisi ujenzi wa TRC, Nastra Chusi mradi wa SGR kipande cha 5 hadi sasa umetekelezwa kwa asilmia 68.28, hivyo elimu hiyo kwa wananchi wa mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga ni endelevu.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment