![]()
Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo mchana wa leo Mei 13, 2025 alipokuwa akizundua Jarida la Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria linalohusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji katika Ziwa Victoria ambapo amesisitiza umuhimu wa kuliweka jarida hilo katika mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa nakala mtandao.
Kadhalika Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa Bodi ya Bonde hilo kwa kuja na mpango wa jarida hilo kwa kuwa athari zinazotokana na Gugumaji hilo ni kubwa na inahatarisha uchumi wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
“53% ya Mkoa wa Mwanza umezungukwa na ziwa Victoria hivyo hapa Mwanza unapozungumzia maji unazungumzia uchumi, sekta ya usafirishaji, uhifadhi wa mazingira na wavuvi pia”.
kwa hiyo madhara ni makubwa sana na elimu hii mliyoitoa kupitia jarida hili ni muhimu sana kwa jamii na ninawapongeza sana kwa kazi kubwa iliyofanyika lakini bado ni endelevu na ni wajibu wetu kihakikisha kuwa ziwa victoria linaendelea kuwa safi. Ameongeza Mkuu wa Mkoa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Dkt. Renatus James Shinu amesema Jarida hilo ni maalumu na limelenga kuhakikisha taarifa muhimu ya shughuli, mbinu, na jitihada ambazo zimefanywa na Serikali katika kupambana na Gugumaji hilo ikiwemo na mipango ya baadae inawafikia Wananchi na Wadau wa sekta ya maji.
Tupe maoni yako





0 comments:
Post a Comment