ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 11, 2025

WAZIRI KIKWETE ATUA PWANI AWAPA MOYO WA UJASIRI WATOTO WA HITIFAKI KUELEKEA UWASHWAJI WA MWENGE WA UHURU APRIL 2

 


VICTOR MASANGU,KIBAHA

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana,ajira na watu wenye ulemavu  Mhe. Ridhiwani Kikwete  leo machi 11 amefanya ziara ya kutembelea na kugagua eneo la uwanja wa shirika la elimu Kibaha ambao utatumiaka katika sherehe za uwashwaji wa Mwenge wa uhuru Kitaifa ambapo baada ya kupita  ameridhishwa  sana  na maandalizi ambayo yanaendelea kufanyika katika uwanja huo.
 Ridhiwani ameyasema hayo wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kutembelea na kugagua  mwenendo na maandalizi katika eneo la uwanja  wa shirika la elimu Kibaha ambapo utakaotimika kwa ajili ya uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ikiwa sambamba na kuzungumza na vijana hao na kuwahimiza kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha maandalizi.

"Nimeridhishwa sana na maandalizi yanayofanyika katika eneo hili la uwanja wa shirika la elimu Kibaha ambapo kutafanyika tukio kubwa la  sherhe za uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa na kwamba nimeweza kuona mwenendo mzima  wa ukarabati wa uwanja huo ikiwa pamoja na kupata fursa ya kuzungumza  vijana wa halaiki,"amesema Ridhiwani Kikwete.

Kadhalika Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wa halaiki ambao  wamechaguliwa kushiriki  katika maandalizi ya uwashwaji wa  Mwenge  wa uhuru Kitaifa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuwa wazalendo na nchi yao na kutunza na kuzilinda rasilimali za Taifa.
Naye  Injinia  kutoka  ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Charles  Kabeho ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa eneo la uwanja utakaotumika  kuwashiwa Mwenge wa uhuru amebainisha kwamba  kwa sasa ukarabati  kwa sasa umeshafikia  asilimia 75.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amebainisha kwamba maandalizi yote kwa ajili ya kuelekea katika  tukio  la kuwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa yanaendelea vizuri katika maeneo ya miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji na kwamba  hadi  sasa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa kwa kiwango kikubwa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kwamba wamejipanga vizuri na kwamba wanatarajiwa kukabidhiwa rasmi uwanja huo amabo utatumika kwa ajili ya sherehe za uwashwaji wa Mwenge wa uhuru Kitaifa na kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Sherehe za uwashwaji rasmi  wa  Mwenge wa uhuru kitaifa  zinatarajiwa kufanyika rasmi Aprili 2 mwaka huu katika viwanja vya shirika la  Elimu Kibaha vilivyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ambapo viongozi mbali mbali wa  ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki katika tukio hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.