NA VICTOR MASANGU,VIGWAZA PWANI..TV..TANRODS
WAKALA wa barabara nchini (TANROAD) Mkoa wa Pwani umewataka baadhi ya madereva wa vyombo vya moto hasa magari makubwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa katika changamoto zao zinazowakabili kuliko kutoa taarifa ambazo sio sahihi kwa kutumia mitandao ya kijamii na kuzua taaruki na sintofahau kwa jamii.
Uongozi wa Tanroad Mkoa wa Pwani umetoa kauli hiyo kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mmoja wa dereva kutoka Kampuni ya Simba logistic Pamela James ambaye alidai kubambikiwa uzito katika mizani ya vigwaza mkoani Pwani tarehe 13 Machi wakati akiwa amebeba mzigo wa kopa akitokea nchini Kongo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment