ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 7, 2024

DC KIBAHA KUZINDUA RASMI SOKO LA KISASA 'KIBAHA SHOPING MOLL' KESHO

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Halmashauri ya Kibaha mji iliyopo Mkoa wa Pwani kesho  inatarajia kuzindua rasmi soka jipya la kisasa linalojulikana kama (Kibaha Shoping Moll) Novemba 7 mwaka huu lililogharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa mapato wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Luna Kakuru  amebainisha kwamba  mradi huo ni kati ya miradi ya kimkakati na kwamba fedha hizo zimetolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan

Luna amesema kwamba katika mradi huuo  wanategemea baadae mapato kuongezeka zaidi kutokana na huduma zitakazoendelea kutolewa ikiwepo maeneo ya maegesho ya magari.


 Naye Afisa Masoko wa soko hilo Sabrina Kikoti amesema katika ufunguzi huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John na mradi huo unaokwenda kutoa huduma nyingi  huduma nyingi ambazo wananchi walikuwa hawazipati kwa wakati.

Amesema katika ufunguzi huo wafanyabiashara mbalimbali wakubwa watashiriki wakiwemo wasanij kutoka ndani na nje ya Mji wa Kibaha.

Nao baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Charles Chandika  amesema kwamba uwepo wa soko hilo ni fursa kwa wafanyabiashara kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mji huo kwa gharama nafuu.

Naye Lidya Vicent mfanyabiasha wa nguo katika soko hilo amesema uwepo wa soko hilo umewawezesha kupata fursa ya mahali sahihi pa kuuzia bidhaa zao .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.