ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 13, 2024

HEKO MAKONDA TUME IMEONGEA NA WANANCHI.

Leo tarehe 13/3/2024 hapa Sapiwi wilaya ya Bariadi tumepokea tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu kufuatia agizo la Mwenezi Paul Makonda Putin. Ikumbukwe kuwa kulikuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na chuo Cha IFM kufuatia upanuzi wa chuo uliopelekea kutwaliwa kwa maeneo ya wananchi kwa fidia ndogo bila kufuata utaratibu. Wananchi walipeleka kilio chao kwa Makonda alipofika mkoani Simiyu na kusikiliza kero hiyo na kuona kweli wananchi wanapunjwa na kuamuru mkuu wa mkoa aunde tume. Leo tume imefika kijijini na kuongea na wananchi ili kusikiliza kero,wananchi wameongea kwa uwazi na tume imekuwa makini sana kusikiliza na kutembelea maeneo kujionea uhalisia. Tume imeahidi kutoa ripoti yenye haki,usawa na isiyomuumiza mwananchi mnyonge. Tunasubiri kupokea majibu ya furaha kwani mkuu wa wilaya alibeza wananchi hao akisema wamewekwa TEGESHA wakati chuo kimewakuta pale. HEKO MAKONDA kwa kujali wanyonge.Heko serikali sikivu ya mama Samia

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.