Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari akieleza matukio mbalimbali yaliyotokea mkoa wa Iringa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha baadhi ya namba za magari na Pikipiki zilizokamatwa ambazo zinasadikika zimetolewa bila kufuata sheria na taratibu za nchi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha baadhi ya leseni zilizokamatwa ambazo zinasadikika zimetolewa bila kufuata sheria na taratibu za nchi.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
JESHI la polisi mkoa wa Iringa linawashikiria wafanyakazi wa TRA Upendo Msigwa mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa mawelewele na Chali Chaliga mwenyewe umri wa miaka 28 mkazi wa Donbosco kwa kosa la kutoa leseni bila kufuata sheria na taratibu za nchi zinavyotaka.
Akizungumza na waandishi wa habari Iringa, Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa wafanyakazi hao wa TRA wamefanya kazi kinyume na sheria hivyo jeshi la polisi linawashikiria na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
ACP Bukumbi alisema kuwa jeshi la polisi liliwakamata Omary kibao miaka 38, Johnson Kihongosi miaka 31na Dikson Nelson 32 kukutwa na leseni za udereva 31,vitambulisho vya Nida na mpiga kura 04,nakala za gari ya watu mbalimbali na Police loss report.
Aidha Kamanda ACP Bukumbi alisema kuwa watuhumiwa hao walikuwatwa na namba za magari na Pikipiki 431,TIN numbers 08, printer 05, laptop 1na desktop 1,nakala za vyeti vya mafunzo ya udereva 02,scaner 01 na lamination mashine 1.
Lakini jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa ushirikiano na askari wa uhifadhi kutoka hifadhi ya Taifa Ruaha wamefanikiwa kumkamata Madambo Nyambinga miaka 27 baada ya kukutwa na silaha moja aina Gobore iliyotengenezwa kienyeji ikiwa imehifadhiwa ndani ya gogo pori la Liyangoro lililopo Kijiji cha Idodi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.