Sostenes Bahati Soka, Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro amesomeshwa mashtaka matatu katika Mahakama mbili tofauti.
Padri huyo mwenye miaka 41, amesomeshwa mashataka hayo leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kwa nyakati tofauti akianza na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kisha Mahakama ya Wilaya ya Moshi.
Kesi ya kwanza ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha ambapo Padri huyo anakabiliwa na shtaka moja la kumbaka mtoto wa miaka 12.
Wakili wa Serikali, Kasimu Nasiri amesema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika
Mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo huku Wakili wa Serikali, Kasimu Nasiri akisema upelelezi umekamilika na Hakimu Salome ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, 2022 ambapo atafikishwa kusomewa maelezo ya awali.
Mshtakiwa huyo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wakazi wa Kilimanjaro ambao wawe na uwezo wakuweka bondi ya Sh10 milioni, kika mmoja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.