ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 26, 2022

KUHIFADHI KINYESI CHAKO KUTAOKOA MAISHA YAKO SIKU ZIJAZO.

 


Kila mara, sayansi hutoa utafiti ambao mwanzoni hukosa kukumbatiwa vyema na kuonekana kana kwamba hauwezekani. Kuweka kinyesi chako kwenye benki kunaweza kuokoa maisha yako katika siku zijazo. 

 Katika utafiti wa sasa, wataalam wa utabibu wamezua gumzo kuhusiana na mpango wa kuhifadhi kinyesi kwa sababu za kiafya. 

Ufafanuzi wa msingi wa kisayansi wa kushinikiza kuhifadhiwa kwa kinyesi ni kwamba matumbo ya binadamu yamejaa vidudu vidogo, au microbiota ambavyo hutoa faida za kiafya. Viumbe hivyo pia wakati mwingine husababisha magonjwa. 

 Baadhi ya utafiti umeonyesha kuwa upandikizaji kwa kutumia vijidudu vya kinyesi, kunaweza kutibu magonjwa fulani vyema kuliko kutumia dawa za viuavijasumu(antibiotics).

 Hivyo basi, wazo la kuhifadhi kinyesi chako ni kutokana na mitindo yetu ya maisha ambapo mambo mengi tunayofanya yanaweza kuvuruga microbiota ya utumbo kwa mfano mlo duni na matumizi ya antibiotics ya kawaida. 

Hii ina maanisha kwamba utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa kadiri maisha yanavyosonga mbele. Kulingana na Daktari Alfred Murage ambaye ni Mshauri Mtaalamu wa Magonjwa ya Wanawake na Mtaalamu wa Uzazi, njia ya kuzuia kuvurugika kwa microbiota ya matumbo ni kuhifadhi kinyesi mapema maishani, au wakati wowote unaofaa unapozeeka. 

Kama wasemavyo akiba haiozi, kinyesi kilichohifadhiwa kinaweza kukusaidia katika siku za usoni kwa kupandikizwa ndani yako. 

Hii inaweza kutibu hali zinazoweza kurekebishwa ambazo zinaweza kutokea baada ya muda. Pengine wajiuliza je, ni wapi unaweza kuweka kinyesi chako? Benki kadhaa za kinyesi tayari zipo, na huenda zikapatikana hivi karibuni mahali popote ulipo. 

Benki za kinyesi sio tofauti sana na benki zilizopo za damu, manii, mayai na aina zote za benki za viungo za mwili. 

Utakapokumbatia wazo la kuhifadhi kinyesi chako, mwanzo utatoa sampuli ya kinyesi kwa uchunguzi katika benki iliyo karibu na wewe. Kinyesi hicho kikitimiza vigezo vya kuhifadhiwa kwa benki, kitashughulikiwa kwa ajili ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu. 

Unaweza kurejelea sampuli yako uliyohifadhiwa kwenye benki iwapo utahitaji. Utafiti wa sasa wa kuhifadhi kinyesi umefufua matumaini hata hivyo kuna changamoto nyingi. 

Moja ya changamoto kuu ni hakuna uhakikisho kwamba sampuli yako ya kinyesi iliyohifadhiwa itaendelea kuwa ya maana katika siku za usoni. 

Pili, hifadhi ya sasa ni ya kudumu takriban miaka miwili. Gharama na udhibiti ni jambo lingine na pia hakuna hakikisho kwamba kurejesha microbiota ya utumbo kwa hali ya awali isiyo na magonjwa kutaimarisha afya. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.