Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akizundua kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa wakilisiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati wa uzizunduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa wakilisiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati wa uzizunduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa
wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewataka walimu wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wanaowafundisha
ili taifa liweze kupata wasomi wengi ambao wanauwezo wa kuja kukisaidia Taifa
hapo baadae.
Akizungumza wakati wa kuzindua vitabu
vyenye muongozo wa waziri mkuu namna ya kuwapata viongozi katika njia sahihi
ambayo haitakuwa na ubabaishaji, Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
alisema kuwa Kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakiaribu taswira halisi ya kada ya
ualimu.
Moyo alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya walimu kufanya mapenzi na wanafunzi na kuwafanyia ukatili wanafunzi kwa makusudi hivyo walimu wanapaswa kutoa taarifa kwa mwalimu yeyeto atakayekutwa anafanya vitendo vya ukatili.
Alisema kuwa kazi kubwa ya mwalimu ni
kuwafundisha wanafunzi waweze kufaulu na sio kuwafanyia ukatili wanafunzi.
Lakini pia mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa vitabu vya muongozo vinataka wateuliwa wateuliwe kwa kufuata misingi sahihi na sio kwa njia ya rushwa au kujuana.
Moyo alisema kuwa muongozo huo
utumike vile ambavyo unastahili kulingana na maagizo ya waziri mkuu Kassim
Majaliwa yanayotaka kuwa na yawe hivyo hivyo.
Aidha Moyo alimazia kwa kusema kuwa
walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa wanafanya vizuri kwenye
kufundisha wanafunzi ndio maana matokeo yake yamaekuwa mazuri mwaka hadi mwaka.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya
Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa walimu wanafanya kazi kubwa kuwafaulisha
wanafunzi licha ya kuwa wanakabiriwa na changamoto mbalimbali hasa mazingira
wanayofanyia kazi.
Ngwada alisema kuwa Halmashauri
inatamani kumaliza changamoto zote za walimu hasa kuboresha miundombini ya
kufundishia na mazingira wanayoishi lakini kikwazo kikubwa kwao ni ufinyu wa
bajeti ambayo wanayo.
Alisema kuwa wakifanikiwa kupata
bajeti basi watakuwa wanatatua changamoto kadili wanavyoweza ili kuwasaidia
walimu kufundisha katika mazingira mazuri.
Awali akisoma muongozo huo kwa mkuu
wa wilaya ya Iringa,kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Gerald Mwamuhamila alisema kuwa kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa
Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi
wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa.
Mwamuhamila alisema kuwa Viongozi wa
Elimu ni nguzo muhimu katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji.
Hivyo Uteuzi wa Viongozi hawa hupaswa
kufanywa kwa Umakini Mkubwa kabla ya kuwakabidhi dhamana ya Kuongoza.
Alisema kuwa Mwongozo huo umeunda
kamati zitakazoshughulikia na Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi
ngazi ya Mkoa. Kabla ya Mwongozo huu Viongozi wa Elimu walipendekezwa na
Kuteuliwa na kamati ya watu wachache Tofauti na itakavyokuwa sasa.
Mwamuhamila alipongeza kuwa Mwongozo Umebainisha Sifa za Kimuundo na Sifa za utendaji wa Kila Cheo cha Uteuzi.
Aidha kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa kitabu cha Mkakati wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji ngazi ya Elimumsingi kimefafanua jinsi ya kuboresha Elimu ya Msingi na Sekondari kwa kuweka Mikakati thabiti yenye kutekelezeka. Kitabu hiki kimetoa hali ya Elimumsingi Nchini, Mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimumsingi, Usimamizi,ufuatiliaji na tathmini ya mikakati, Ushiriki wa wadau katika kufanikisha utekelezaji wa mkakati.
Kitabu cha tatu utakacho kizindua leo ni kitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimumsingi na Kitabu hicho kimebainisha Changamoto, hatua za kuchukua ili kukabiliana na changamoto hizo, pamoja na kubainisha kinachotakiwa kufanyika ili kushirikisha wasimamizi wa Elimu, Wazaz/Jamii, Viongozi na wadau mbalimbali kuhusu usimamizi madhubuti wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari.
Lakini pia hatua zilizobainishwa zinakusudiwa kutumiwa kama mwongozo kwa Viongozi katika ngazi zote Taifa, Mkoa, Halmashauri, Kata, Kijiji,Mtaa na Shule katika utatuzi wa changamoto zinazokwamishaufundishaji na ujifunzaji
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.