Mhifadhi mkuu Msaidizi Tarafa ya nne Mgololo,Lukiko Maiila akiongea na waandishi wa habari wakati wa usahili wa vijana 49 wa kupandana na majanga ya moto katika shamba lamiti la Sao Hill
Baadhi ya vijana waliojitokeza wakiwa kwenye usahili uliofanywa katika kijiji cha Kitasengwa kata ya Makungu
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
WAKALA wa huduma za
misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti ya kupanda na asili la Sao Hill Mkoani
Iringa wilaya ya Mufindi wamesema majanga ya moto yamepungua kutokana na elimu
ambayo wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara juu ya madhara yanayotokana moto.
Akizungumza wakati wa
usahili wa vijana wa kupambana na moto Mhifadhi mkuu Msaidizi Tarafa ya nne
Mgololo,Lukiko Maiila Alisema kuwa wamekuwa wanaajili mara kwa mara wafanyakazi
kwa ajili ya kupambana na moto katika tarafa hiyo.
Maiila Alisema kuwa
wamekuwa wanasaidia kuzima na kupambana na moto kipindi ambacho kunakuwa
kimetokea kwa majanga hayo.
Alisema kuwa moto
umekuwa unaleta madhara ya kiuchumi kwa shamba la Sao Hill na wananchi ambao
wamekuwa wanalima mazao ya misitu.
Maiila alisema kuwa
wamekuwa wanatoa elimu mara kwa mara juu ya madhara ya moto kwa wananchi wote
wanaolizunguka shamba la miti la Sao Hill.
Alisema kuwa
wamefanya usahili wa vijana mia moja thelethini na saba (137) kutoka Vijiji
kumi na mbili (12) na wanaotakiwa kuajiliwa ni vijana 49 katika Kijiji cha
Kitasengwa kata ya Makungu.
Maiila alisema kuwa
wamefanya usahili wa ukakamavu kwasababu maeneo ambayo wanaenda kufanyia kazi
yanamiinuko mingi hivyo walipokuwa na utimamu wa mwili hataifanya kazi
inavyotakiwa
Alisema kuwa tarafa
ya nne ya shamba la Sao Hill wanatarajia kuajili wafanyakazi 2000 ambao
watakuwa wanafanya kazi mbalimbali katika tarafa hiyo kwa lengo la kulinda na
kuitunza miti ambayo ipo katika shamba la Sao Hill.
Maiila alimazia kwa
kusema kuwa hawatarajii kupata majanga ya moto katika kipindi hiki cha kiangazi
ambacho mara nyingi majanga hayo ndio hujitokeza.
Kwa upande wake
baadhi ya wananchi wanaolizunguka shamba hilo wamesema kuwa limesaidia kutoa elimu
ya madhara ya moto na kupunguza majanga ya moto kutokea mara kwa mara.
Walisema kuwa elimu
ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara imesaidia wananchi wengi kuwa na uelewa
mpana wa namna gani ya kuzuia kusitokee janga la moto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.