Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Theresia Mtewele wakigawa viti kwa ajili ya walemavu mkoani Iringa
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Theresia Mtewele wakigawa viti kwa ajili ya walemavu mkoani Iringa
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Theresia Mtewele wakigawa vifaa kwa ajili ya walemavu mkoani Iringa
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Theresia Mtewele na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati wakizundua mchezo wa mpira wa kikapu wakati wa kongamano la watu walemavu mkoani Iringa
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Theresia Mtewele na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati wakizundua mchezo wa mpira wa kikapu wakati wa kongamano la watu walemavu mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa
Mhe. Rita Kabati na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha
mapinduzi (CCM) Theresia Mtewele wameungana
kwa pamoja kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa watu wenye ulemavu mkoani
Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Akizungmza wakati wa Kongamano maalum lililolenga kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kutoa
elimu ya Sensa ili kuwajengea uelewa na kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la
Sensa linalotarajiwa kufanyika Mwezi nane Mwaka huu,MNEC Mtewele alisema kuwa matukio
ya ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa yamekuwa yakitokeza mara kwa mara hivyo
ni lazima kuyakomesha matukioa hayo.
MNEC Mtewele alisema kuwa wananchi wa
Iringa wanapaswa kutambua madhara yanayotokana na ukatili wa kijinsia kwa jamii
husika kwa kuwa kumfanyia mtu ukatili ni jambo ambalo halikubariki katika jamii
yoyote ile ya kitanzania.
Alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Mkoa huo unaongoza kwa ukatili wa kijinsia na
kwamba jamii yote hususani wakazi wa Mkoa huo wanapaswa kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutokomeza vitendo hivyo kama
anavyofanya Mbunge Kabati.
“Ni aibu sana na fedheha kwa mkoa
wetu kuongoza katika vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunapaswa kupiga vita kwa
nguvu zetu zote na mtu akikutwa na hatia ya kuhusishwa na vitendo hivi anapaswa
kuchukuliwa hatua kali hata kufungwa maisha” alisema MNEC Mtewele huku
akionesha kukasirishwa na vitendo hivyo.
katika hatua nyingine amezungumzia
umuhimu wa watu wenye ulemavu kushiriki katika Sensa ya watu na makazi
inayotarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu na kuhimiza kuhesabiwa kwa watu
wenye ulemavu na kwamba zoezi hilo litaifanya Serikali kutambua idadi ya
watu hao na hivyo kupata huduma kwa urahisi kutokana na mahitaji yao na maeneo
walipo.
“Ndugu zangu naomba sana kuhamasisha
wazazi na walezi kuhakikisha watu wote wenye ulemavu tulinao majumbani
wanahesabiwa, usimfiche mtu mwenye ulemavu kwani kwa kufanya hivyo utaifanya
Serikali kukosa idadi yao na hivyo kushindwa kuwafikia kuwapatia huduma zao wanazostahili” amesisitiza
MNEC Mtewele
MNEC Mtewele alimazia kwa kumpongeza Mbunge Ritta Kabati kwa hatua yake ya kusaidia watu wenye mahitaji maalum na kwamba kwa kufanya hivyo anaunga mkono jitihada za Serkali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto na walemavu.
Awali akizungumza wakati wa kongamano
hilo mbunge DR Ritta Kabati alisema kuwa imekuwa ni ndoto na kiu
yake ya muda mrefu pia imetokana na kushuhudia changamoto nyingi wanazokumbana
nazo watu wa makundi maalum hususani wenye ulemavu, wazee, watoto, yatima
na wanawake ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa
Jamhuri a Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kupinga ukatili wa
Kijinsia.
“Mgeni Rasmi kutokana na changamoto hizo nilianza
kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha napunguza au kuondoa changamoto hizo kabisa”
alisema DR Kabati
Alisema kuwa amekuwa akiuliza mara
kwa mara maswali na hoja zinazohusu watu wenye Ulemavu Bungeni ili kutafuta ufumbuzi
ikiwemo mabadiliko ya kisheria na sera mbalimbali kuendana na mazingira yao.
Dr Kabati alisema kuwa aliamua
kuanzisha kampeni maalum ya kusaidia vifaa saidizi ikiwemo fimbo, basikeli,
mafuta na hata kuboresha miundombinu katika baadhi ya maeneo ili wasikutane na
changamoto hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa baada ya kuona
hali ya uhitaji katika jamii ni kubwa, aliamua kuanzisha Taasisi maalum ya
kushughulikia changamoto zinazowakabili watu waliopo kwenye makundi
maalum inayoitwa RITTA KABATI TRUST FUND, ambayo itajihusisha moja kwa moja
kutafuta ufumbuzi wa changamoto za watu wenye mahitaji maalum kwa kuwafuata
kwenye maeneo yao na kuwatambua ili kufanya uratibu wa kuwasaidia.
“Taasisi hii inalenga Kukuza utu na heshima kwa watu wenye ulemavu na kutoa ushauri wa matibabu
bila malipo kwa walemavu pamoaja na kusaidia miradi na shughuli nyingine za
kiuchumi zinazoendeshwa na watu wenye ulemavu” alisema DR Kabati.
Aidha amebainisha kuwa kazi nyingine
ni kuanzisha na kudumisha vituo vya walemavu ili kusaidia
jamii na kujihusisha katika michezo hususani ya watu wenye ulemavu kwa kuanzisha mashindano mbalimbali ya michezo na burudani katika Mkoa wa
Iringa.
Kazi nyingine ni pamoja na kusaidia programu na mipango inayolenga kuwaelimisha na kwafahamisha wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kuhusu changamoto mahususi zinazowakabili watoto wenye ulemavu na jinsi ya kuwatunza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.