ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 19, 2022

Dkt ANGELINE ATOA VIFAA KWA CCM WILAYA YA ILEMELA

 Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula ametoa vifaa mbalimbali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela,ili kuimarisha chama hicho pamoja na kuhakikisha uchaguzi ndani ya chama unaenda vizuri.

Dkt Angeline ametoa vifaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi wa viongozi mbalimbali ndani ya chama hicho kwa Wilaya hiyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 12(12,848,000) ikiwemo Ream 582 zenye thamani ya shilingi 8,148,000, Kalamu boksi 20 zenye thamani ya shilingi 260,000. Pia ametoa vifaa vingine kwa ajili ya kuimarisha chama kama ikiwemo luninga mbili kwa makada wa vijiwe vya Kahawa vya Kata ya Kirumba na Mwigulu Kawekamo vyenye thamani ya shiling 630,000, bati 22 kwa ajili ya kupaua ofisi ya CCM Kata ya Kahama zenye thamani 480,000,gharama za usafiri kwa Wakurugenzi wa uchaguzi wa Kata 19,matawi 126 na jumuiya zao jumla milioni 3.33(3,330,000). Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Dkt. Angeline amesema ameamua kutekeleza zoezi hilo kama sehemu ya wajibu wake kwa chama hicho pamoja na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM taifa na Samia Suluhu Hassan katika kuwarahisishia watendaji wa chama hicho kutekeleza zoezi la uchaguzi kwa amani, haki na uhuru

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.