Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Zuhura Yunus Abdallah kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu kabla ya uteuzi huo, Zuhura alikuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
Zuhura anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine na uteuzi huo umeanza Januari 30, 2022.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.