ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 21, 2019

UPEKEE WA WAZIRI ALIYETEMWA NDIYE ALIYECHUKUWA NAFASI YA JANUARY MAKAMBA

George Simbachawene.
 Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanioa Dkt John Pombe Magufuli amemteua Mbunge wa Kibakwe George Simbachawene kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya January Makamba.

Uteuzi huo wa Rais Magufuli unamfanya Simbachawene kuweka rekodi ya kuwa Mbunge pekee ambaye alijiondoa kwenye Baraza la Mawaziri na kurejea tena baada ya miaka miwili.

Septemba 06. 2017 akiwa Waziri wa TAMISEMI, Simbachawene alitajwa kwenye ripoti ya Uchimbaji wa madini ya Tanzanite, na Almasi kupitia Kamati ya Bunge, ripoti ambayo iliwasilishwa kwa Spika Ndugai na yeye kumkabidhi Waziri Mkuu Majaliwa ili aipeleke kwa Rais Magufuli.

Septemba 06. 2017 baada ya ripoti hiyo kukabidhishwa kwa  Rais Magufuli, Simbachawene alitangaza kujiuzulu nafasi Uwaziri wa TAMISEMI ili kupisha tuhuma dhidi yake.

Agosti 28, 2018, Simbachawene alichaguliwa na Wabunge wenzake kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi Hawa Ghasia ambaye alitangaza kujizulu.
Aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.