ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 25, 2019

WILAYA YA MISUNGWI SASA KUSAHAU ADHA YA MAJI


WATU zaidi ya 64,000 wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji safi na salama pindi mradi wa maji unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira utakapokamilika wilayani Misungwi mkoani Mwanza

Uzalishaji wa maji unatarajiwa kuongezeka kutoka lita za ujazo 650 kwa siku hadi kufikia mita za ujazo 4500 kwa siku sawa na ongezeko la asilimia 85.5.


"Mheshimiwa rais alipokuja hapa aliwaahidi kwamba miradi yote hii ya maji itakamilika kwa kipindi kifupi" Alisema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Kassim majaliwa na kuongeza


"Ni wahakikishieni Mhe. Mweyekiti ule mradi wako wa maji. Serikali  tulikuwa tukiendelea kukusanya fedhs hizo milioni 600 tunazo, tutamlipa mkandarasi milioni 400 kwa haraka sana halafu fedha iliyobaki yaani milioni 200 atalipwa atakapokamilisha kazi" alisema majaliwa.

Serikali imeweka malengo kuwa ifikapo mwezi wa sita mradi huo umekamiliaka.
PMO_9553
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa   (kulia) wakimsikiliza, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji  na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) alipotoa maelezo kuhusu ujenzi wa Mradi wa Maji na Usafi  wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. 
………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza ihakikishe inafanya msako wa watu wote waliohusika na wizi wa fedha na vifaa katika eneo la ujenzi wa mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Misungwi mkoani Mwanza.
 Ametoa agizo hilo Jumanne, ya mwezi Machi 19, 2019 wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira uliopo wilayani Misungwi, ambapo ametumia fursa hiyo kuiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza iimarishe ulinzi katika eneo la mradi huo.
 Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya uvamizi wa mara kwa mara kwenye eneo hilo la mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Nyahiti wilayani Misungwi, Mwanza.
 “Hawa waliofanya tukio hilo la uvamizi katika eneo la mradi si tu wanamuhujumu mkandarasi na kampuni yake, bali wanahujumu jitihada za Serikali ili miradi ya maendeleo kwa wananchi isikamilike hatutakubali, wananchi tushirikiane katika kuwabaini wote waliohusika.”
 Ujenzi wa mradi wa maji katika mji wa Misungwi ni utekelezaji wa Sera ya Maji pamoja na Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 inayoelekeza Serikali kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 95 wakazi waishio mijini na waishio vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.
 Awali,Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi wa maji katika mji wa Misungwi unatekelezwa kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Ziwa Viktoria, ambao unatekelezwa katika miji ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Magu, Misungwi na Lamadi kwa gharama ya Euro milioni 104.5 sawa na wastani wa sh. bilioni 276.
 Amesema katika kiasi hicho cha fedha, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) zinachangia Euro milioni 90 sawa na sh. bilioni 238 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu, ambapo Serikali ya Tanzania inachangia Euro milioni 14.5 sawa na sh. bilioni 38.
 Profesa Mbarawa amesema mradi wa maji na usafi wa mazingira katika mji wa Misungwi unagharimu kiasi cha Euro milioni 4.85 ambazo ni sawa na wastani wa sh. bilioni 12.85 ambazo zinatumika katika ujenzi wa kituo cha uzalishaji na kutibu maji, ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 53.7.
 Pia, fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji yenye ukubwa wa lita 600,000 na lita 300,000, ujenzi wa kituo cha kutibu majitaka, ununuzi wa magari mawili moja la kunyonya majitaka na Toyota pick up na pikipiki mbili pamoja na ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji na nyumba mbili za watumishi katika kituo cha uzalishaji.
 Waziri Profesa Mbarawa amesema mbali na ujenzi huo pia watajenga maabara ya kupima ubora wa maji na karakana ya matengenezo. Mradi huo pia utaunganisha kaya 2,158 katika mfumo wa maji pamoja na kuwafungia mita za maji na ujenzi wa vituo 13 vya kuchotea maji.
 Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) ya China chini ya Mhandisi Mshauri Kampuni ya Egis ya Ufaransa na unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA) ulianza Mei, 2017 na unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.
PMO_9566
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mji  wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. Kushoto  kwake ni Waziri wa Maji, Profesa, Makame Mbarawa na  kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
PMO_9573
PMO_9606
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga kuhusu michoro ya Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi kabla ya kuweka jiwe la msingi la Mradi huo, Machi 19, 2019.  Wa pili kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na wa pili kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda. PMO_9613
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Maji  na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.  Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Daallo. PMO_9630
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua mashine za  za kusukuma maji kabla ya kuweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa  Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. PMO_9651
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteremka kutoka kwenye chujio la maji wakati alipokagua ujenzi wa  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.