ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 19, 2019

MAJALIWA AUPOKEA MWILI WA MAMA YAKE VICKY KAMATA.


Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa mapema asubuhi  ya leo jumanne majira ya saa 3 katika uwanja wa ndege wa Mwanza ameshiriki kuupokea mwili wa marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika katika eneo la mapokezi la uwanja wa Airport Mwanza.

Mhe. Majaliwa yupo jijini hapa kwa ziara yake ya siku tatu aliyoianza jana kwa kufungua Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini kilichofanyika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.

Leo Mhe. Waziri Mkuu ameendelea ziara yake kwa kufungua Ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kanda ya Ziwa na kukabidhi matrekta 16 kwa vyama vya  Ushirika vya Msingi, kisha baada ya hapo ameelekea Kijiji cha Kolomije Wilayani Misungwi kufungua Kituo cha Afya, kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Misungwi kwenye chanzocha maji kilichopo kijiji cha Nyahiti na kuhutubia wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.