ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 22, 2019

"DAWA NI USHINDI TU KWA STARS, TUKIFUATILIA MATOKEO YA CAPE VERDE Vs TUTAPATA MAKENGEZA"



Taifa la Tanzania liko kwenye kampeni ya kusaka ushindi yaani pointi zote tatu za mchezo wa Jumapili dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, lakini wakati huo huo kusonga mbele kwa Stars, kunategemea matokeo ya upande wa pili,  mchezo wa Cape Verde dhidi ya Lesotho.

Mchambuzi wa michezo, mwanahabari ambaye pia kajikita zaidi katika soka Saleh Ally (Jembe) anasema Dawa yake Watanzania wajikite katika kuusaka ushindi tu kwa Stars kwani tukifuatilia matokeo ya Cape Verde tutapata makengeza...... Msikilize wakati akichonga kwa njia ya simu na Gsengo wa kipindi cha KAZI NA NGOMA ya Jembe Fm Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.