Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve akiwa na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Iringa vijijini ambao wamefanikiwa kuunda mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kukuza kipatao chao.
Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve akiangalia vitu vilivyotengenezwa na akinamama ambao tayari amewawezesha
MBUNGE wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve akiongea na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MBUNGE
wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve amefanikiwa
kuunda mfuko wa umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Iringa vijijini ambao
utasaidia kukuza kipata na kuongeza kasi ya maendeleo.
Akizungumza
na blog hii mbunge huyo alisema kuwa amefanikiwa kufanya ziara katika wilaya
Iringa vijijini na kuziwezesha kata zote kwa kutoa shilingi laki sita kwa kila
kata.
“Nimetembea
kata ishirini na nane (28) na kutoa shilingi 600,000 kwa kila kata kwa wanawake
wa UWT ili kukuza uchumi wa jumuiya hiyo ambayo ndio imekuwa nguzo kwa familia
yoyote ile” alisema Tweve
Tweve alisema
kuwa tayari amezunguka katika kata zote 36 za wilaya ya Mufindi na kufanikiwa
kuwawezesha kama alivyo fanya kwenye wilaya ya Iringa vijijini hivyo anajipanga
na kuhakikisha kote huko wanaunda mfuko wa wilaya kwa maendeleo ya wanawake
hao.
“Mimi ni
mbunge ambaye nimechaguliwa na wanawake wa chama cha mapinduzi hivyo ni lazima
nihakikishe nawaletea maendeleo kwa kutumia ubunifu wangu wote na kuhakikisha
wananchi wanaunga mkono juhudi za Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr John Pombe Magufuli” alisema Tweve
Aidha Tweve
alisema kuwa lengo ni kuhakikisha anazifikia kata zote za mkoa wa Iringa na
kuwawezesha akinamama kiuchumi ili kufanya maendeleo kwa kuendana na kasi ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
“Hadi sasa
nimefanikiwa kutoa zaidi ys shilingi milioni 38,400,000 kwa ajili ya
kuwawezesha wanawake wa mkoa wa Iringa ili waweze kukuza vipato vyao vya
kiuchumi” alisema Tweve
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.