ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 21, 2018

DC MURO ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MBUYUNI

Imma Msumba, Arumeru.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni kilichopo katika Halmashauri ya Arusha Dc  ambacho Serikali imetenga fedha Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara na Nyumba ya Mtumishi wa kituo hicho pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 
Dc Muro akikagua ujenzi wa Kituo hicho ameleza kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya kwa kuimarisha huduma za Afya na kujenga vituo vyenye hadhi vijijini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Ujenzi wa Kituo hicho Ndg.Leskara Olerangai Ambaye pia ni Diwani mstaafu wa kata ya Oljoro ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa  kuwezesha kutoa fedha kwa wakati huku akimpongeza Dc Muro kwa jitihada zake anazozifanya ili kuhakikisha ujenzi una kamilika kwa wakati.
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro akiwa ameambatana na wadau wa Kamati ya ujenzi akikagua maendeleo ya shughuli za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni kilichopo katika Halmashauri ya Arusha
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.