ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 13, 2018

NJAA MBAYA MAJANGILI WA WANYAMA PORI SASA WATUMIA NJIA ZA UCHOCHORONI.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA),Twaha Twaibu kushoto akiwa na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa Pori la Akiba Selous Augustine Ngimilanga wakiangalia baiskeli zilizotumiwa na majangiri kubebea wanyamapori.
 Ofisa Kampuni ya uwindaji wa Kitalii ya Mkwawa Hunting Safari Benson Kibonde akisisitiza jambo mbele ya Afisa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA),Twaha Twaibu kushoto na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Magharibi - Msolwa Pori la Akiba Selous Augustine Ngimilanga.
 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea Shule ya Msingi Ukombozi kujionea mchango wa uhifadhi kutoka kampuni za uwindaji wa kitalii. 
 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya  na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani Morogoro baada ya kutembelea jengo la Ofisi ya Kijiji cha Msolwa Station linalojengwa kwa fedha kutoka kampuni za uwindaji wa kitalii. 
 Afisa habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Twaha Twahibu akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa Kijiji cha Msolwa Station kinachopakana na Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa mkoani Morogoro.

KILOMBERO
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika kipindi cha mwaka 2017/18 imekamata baiskeli 60 za watuhumiwa wa ujangiri zikiwamo Nyaya zaidi ya 100 ndani ya Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi- Msolwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi waishio jirani na Pori hilo la Akiba kubuni mbinu zaidi ya kuuwa wanyamapori ambapo sasa wameanza kutumia Vuvuzela zinazotumiwa na mashabiki kwenye michezo hususani mpira wa miguu.
Vifaa hivyo hutumiwa usiku na majangiri wakiwa na tochi ambapo hupuliza Vuvuzela kwa lengo la kuwachanganya wanyamapori huku wakiwa wamewamulika na mwanga wa tochi kisha kuwavamia na kuwakatakata miguu.
Mkuu wa Kanda hiyo, Augustine Ngimilanga akizungumzia zaidi anasema tayari wameweza kukabiliana na aina hiyo mpya ujangiri na kupitia askari wa doria walikamata watuhumiwa wa ujangiri waliofunguliwa kesi 92 zinazoendelea Mahakama ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
“Watuhumiwa 18 wameshasomewa kesi zao na kuhukumiwa baadhi wamefungwa miaka mitatu na wengine miaka tisa jela,” alisema Ngimilanga na kuongeza:
“Tumeweka mkakati wa kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na ulinzi wa doria muda wote, hii ni pamoja na kukabiliana nao kabla hawajaingia na kufanya uharibifu,” alisema.
Ngimilanga alizitaja changamoto katika kukabiliana na ujangiri zinachangiwa na hali ya umasikini ya wananchi katika vijiji vinavyopakana na pori hilo.
“Baadhi ya wananchi wameona njia pekee ya kujipatia kipato ni kufanya ujangiri wa kuwinda wanyama na kuvua samaki kwenye mito ndani ya Pori la Akiba.
“Mbali ya kukamata tunaowakuta, tumeendelea pia kutoa elimu maeneo mbalimbali ya vijiji ikiwamo mikutano ya vijiji kwa kuwaelimisha na kuwapa mifano ya umuhimu wa kutunza haya maeneo,”alisema.
Alisema ili kuwasaidia kutoshiriki vitendo vya kijangiri wamekuwa wakiwapa elimu ya ujasiriamali wa ufugaji nyuki kwa ajili ya kuvuna asali na kuuza kwa lengo la kujiongezea kipato.

“Tumewasaidia kupata ufadhili wa mizinga kutoka kwa wawekezaji ili waendeshe shughuli za ufugaji kwenye msitu wa Magombela,” alisema Ngimilanga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.