ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 10, 2018

HAYA NDIYO MAPINDUZI YA VIWANDA SEKTA YA VITAFUNWA.

Mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mwanza Seif Hussein akikata utepe sanjari na wageni meza kuu, kama ishara ya uzinduzi rasmi wa duka na bakery ya uokaji mikate na keki ya Kela Bakery iliyopo barabara ya Uhuru eneo maarufu Dampo jijini Mwanza.
VIDEO YA TUKIO/GSENGOtV
Mkurugenzi wa Kela Bakery Maruzuku Magongo akikaribisha wageni.
Salaam salaam za wenyeji na wageni tukioni.
Jiografia ya eneo la tukio.
"Bakery hii leo ndiyo inaanza kazi rasmi na ninyi mmekusanyika hapa ili muwe mashuhuda na vionjo vyenu ndivyo vitakavyotupa mwongozo wa kutusaidia pale ambapo tunapaswa kuwako na hili pia ni kupitia tathimini yenu" Hii ni kauli toka kwa Mkurugenzi wa Kela Bakery Maruzuku Magongo

"Hakika nimefarijika sana kwani kitendo cha kufanya utafiti kutembea nchi za wenzetu ambazo zimepiga hatua kimaendeleo na kuja na teknolojia zao kuzisimika hapa hili ni jambo kubwa la kuigwa na wengine" asema Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mwanza Seif Hussein na kisha kuongeza "Ni matumaini yangu kwamba kiwanda hiki cha Kela Bakery kitakuwa mfano katika jiji hili la Mwanza kwa uzalishaji bidhaa bora na tunategemea kuonja ladha tofautitofauti" 
Kusanyiko la hafla hii ya uzinduzi.
"Ndani ya uwekezaji huu siyo tu kwamba tunafungua fursa za ajira na kwa vijana wetu wenye fani zao za masuala ya mapishi kuajiriwa hapa bali pia uwekezaji huu ni tafsiri ya Serikali ya Viwanda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Magufuli ambayo ni dhana pana, haiishii tu katika uzalishaji wa bidhaa ngumu bali pia unaingia hadi uzalishaji na usindikaji wa vyakula"
Kwa umakiiiiiini......
Magongo Jr ndiye aliyekuwa Mc wa hafla hiyo.
Kela Bakery.
Vitu adimu...
Ladha yako sasa iko mezani kwako.
Keki kila aina.
Chocolate, ice cream, fruits nakadhalika
Mikate.
Vyakuoka vyote viko hapa.
Chocolate Muffin, bagia, samosa na biskuti.
Cake kwa hafla zote utapata Kela Bakery iliyopo barabara ya Uhuru Dampo jijini Mwanza.
The cake.
Wow......................
Kutamani ruksa ila hakikisha one day inatua mezani kwako..............
Iwe za pilipili na zisizo..............
Egg chop.............
Mikate ya kale..............
Mikate ya ngano isiyokobolewa pia yapatikana........
Karibuni............
Keki ya uzinduzi imetua mezani.
KARIBU SANA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.