Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa waliopo Shule ya Polisi Moshi zamani CCP wakati wa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua gwaride baada ya kuwasili Shule ya Polisi Moshi zamani CCP kwa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamis Issah na RPC Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ramadhan Nganzi wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli wakati alipokwenda kuzungumza nao wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoa wa Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli katika mkutano wa hadhara wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi. Theresia Mhongo wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi)
Na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa majambazi na wahalifu
wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha mara moja kabla ya kukutana
na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo pia ametoa wito kwa wazazi kuwakanya
watoto wao kujihusisha na vitendo hivyo.
IGP Sirro ameyasema
hayo wakati akizungumza na Wakazi wa Mto wa Mbu Tarafa ya Manyara Wilayani
Monduli Mkoani Arusha wakati wa Ziara yake mkoani humo yenye lengo la kubaini
changamoto za kiuhalifu na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema hivi sasa
ujambazi wa kutumia silaha umepungua kwa kiasi kikubwa na baadhi ya matukio
ambayo yamekuwa yakijitokeza yanaendelea kudhibitiwa na Jeshi la Polisi.
“Nawasihi
wanaofikiria kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo vya utumiaji wa
silaha na kuua watu waache mara moja kwa kuwa wakikutana na moto wa Jeshi la
Polisi wasije wakajilaumu mana kwa sasa moto wetu ni mkali hivyo nawashauri
wazazi wakanye watoto wao” Alisema Sirro.
Aidha amewataka
Wakazi wa Mto wa mbu Wilayani Monduli kuendelea na shughuli zao kama kawaida
kwa kuwa usalama umeimarishwa katika kupambana na wahalifu waliokuwa wakifanya
vitendo vya kuwaua watu hususani wanawake ambapo katika kipindi cha hivi
karibuni kuliripotiwa matukio kadhaa ambayo yalileta wasiwasi katika eneo hilo
muhimu kwa utalii.
Amewataka Viongozi wa
Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa suala zima la ulinzi na usalama linatiliwa
mkazo ili kuhakikisha hakuna mhalifu katika maeneo yao na wageni wanapoingia
wachukue taarifa zao mapema.
Kwa Upande wake Afisa
Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Bi. Kuluthum Hassan alisema Wahalifu wanaouza
bangi, pombe ya gongo na dawa za kulevya wanaendelea kuwafichua ili wafikishwe
katika vyombo vya dola na hivi sasa wanaendelea na mipango ya ujenzi wa kituo
kikubwa cha Polisi kitakachoendana na hadhi ya eneo hilo.
Nao wananchi
mbalilmbali wa Mto wa mbu wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha kuwa
maeneo hayo yanakuwa salama wakati wote hususani kipindi hiki cha watalii wengi
katika maeneo hayo na wameahidi kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi ili
kuboresha usalama katika eneo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.