ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 21, 2018

PICHA ZA MAZISHI YA MAREHEMU MONICA POMBE MAGUFULI

MWILI wa Dada wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Marehemu Monica Magufuli umezikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita leo Jumanne.

Viongozi mbalimbali wa serikali, siasa na dini wakiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mkewe, Bi. Mary Majaliwa, wabunge, Mama Salma Kikwete, RC Paul Makonda wameungana na familia ya Magufuli katika kumsindikiza Monica kwenye nyumba yake ya milele.

Bi. Monica alifariki dunia Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Bugando alikokuwa amelazwa akipatiwa matuibabu.Jenerali Mabeho akisaini kitabu cha maombolezo kwa msiba wa dada wa Mhe.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
IGP Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo kwa msiba wa dada wa Mhe.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Valentino Mloholo Mkurugenzi wa Takukuru Tz akisaini kitabu cha maombolezo kwa msiba wa dada wa Mhe.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.