ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 24, 2018

VIDEO:- MMILIKI WA KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA JIJINI MWANZA ATIWA MBARONI KISA HIKI HAPA.



GSENGOtV

Ni kama kutimia kwa ule msemo usemao 'MBUZI KAFIA BUCHANI' kwani wakati Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akirejea kutoka ziarani  kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Serikali iliyo ndani ya mkoa wake, baada ya kuikamilisha kwa siku yake ya kwanza, wilayani Magu, akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, yanatokea yakutokea.

Mongella na msafara wake wanapita katika kiwanda cha kuchambua Pamba, kukamua na kuzalisha mafuta cha ICK na kuwakuta maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)  wakimhoji Mkurugenzi wa kiwanda hicho BAWESHI CHANDULARI GANDECHA kwa kosa la kutumia malighafi zenye kemikali zilizo mahususi kwa viwanda vya utengenezaji nguo, karatasi, kutibu majitaka ya vyoo na matumizi mengine yasiyo ya chakula, badala yake yeye akitumia kemikali hizo kutengeneza mafuta ya kula na ndipo habari inapo badilika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.