ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 28, 2018

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CHATEUA MAJINA MAWILI.Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kinachoendelea kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli kimepitisha majina mawili ya wajumbe wapya wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na NEC.

Wajumbe hao ni Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu nne Mizengo Peter Pinda pamoja na Makongoro Nyerere.

Kikao hicho pia kimepiga kura ya kuwapata wajumbe sita kwa kuzingatia jinsia, watatu kutoka Tanzania Bara na watatu kutoka Tanzania Zanzibar ambao watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Jumla ya majina 18, tisa kutoka kila upande yalipendekezwa kuwania nafasi hizo.

Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere waliteuliwa na  Rais Dkt. Magufuli  hivi karibuni kabla siku ya leo Mei 28, 2018 kupitishwa rasmi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.