ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 2, 2018

MBELE YA WEMA! Diamond na Mobeto Wakumbatiana Live!


MBELE YA WEMA! Diamond na Mobeto Wakumbatiana Live! Zile tuzo zilizokuwa zikiwaniwa kwa muda mrefu za 'Sinema Zetu International Film Festival' zilizoandaliwa na kituo cha Azam Tv, hatimaye zimefikia tamati na wasanii mbalimbali wa filamu wamejitokeza katika ukumbi wa Mlimani City, kwa ajili ya kushuhudia nani ataibuka kidedea na kujinyakulia tuzo katika vipengele tofauti tofauti. Katika usiku huo wa ugawaji wa tuzo za SZIFF, watu maarufu kutoka katika tasnia mbalimbali na viongozi wa serikali walijitokeza, akiwemo mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na mzazi mwenziye Hamisa Mobeto, ambao waliitwa jukwaani kwa ajili ya kutoa tuzo kwa mshindi. Baada ya kupanda jukwaani Hapo Diamond na Mobeto walikumbatiana na mbongo fleva huyo akatoa maneno matamu ya mahaba kwa mama mtoto wake huyo, huku Malkia wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, akishuhudia tukio hilo live, hali iliyozua minongo'no kwa wageni waalikwa waliofika ukumbini hapo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.