Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akitoa taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa
Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo Mtaa wa Relini-Kizota Mjini Dodoma, Jana 21 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-NRFA
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini inazidi kuimarika huku
serikali kupitia wizara ya kilimo ikiwa imejipanga kukabiliana na changamoto ya
uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao mbalimbali hususani mahindi.
Katika taarifa ya Bi
Vumilia L. Zikankuba Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula katika
hafla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi
wa vihenge na maghala ya kisasa katika Mtaa wa Relini-Kizota Mjini Dodoma
aliyoitoa mbele ya mgeni rasmi-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Kassim Majaliwa (Mb) jana tarehe 21 aprili,
2018 alieleza kuwa mradi huo pindi utakapokamilika
utafungua fursa kubwa kwa wakulima nchini.
Alisema
kuwa Baada ya Mradi huu kukamilika uwezo wa kuhifadhi wa Wakala wa Taifa wa
Kuhifadhi Chakula utakuwa mara mbili ya uwezo wa sasa yaani kutoka tani 251,000
hadi tani 501,000 huku ikitarajiwa kufikia Tani 700,000 kufikia mwaka 2025.
Bi Vumilia alieleza
kuwa Mikataba ya mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula, ilisainiwa na
kuanza kazi tarehe 09 Desemba 2017 kati ya (NFRA) na makampuni mawili toka
nchini Poland ambayo ni Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o. Aidha, mradi
huo utatekelezwa kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 55 na unatarajiwa
kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na nane (18) kuanzia mwezi Mei 2018.
Maandalizi
ya awali ya mradi huo yalifanywa na kampuni kutoka nchini Poland iliyofanya
upembuzi yakinifu wa awali na kupendekeza gharama za mradi kuwa dola za
kimarekani millioni 55 ambazo zingetosheleza kujenga vihenge vyenye uwezo wa Tani
150,000 na maghala yenye uwezo wa Tani 50,000, hivyo kufanya uwezo wa jumla wa
mradi kuwa Tani 200,000.
Alisema,
ili kujiridhisha zaidi Wakala kupitia Wizara mama, iliunda timu ambayo ilifanya
upya tathmini ya mradi na kupata thamani halisi ya mradi (value for money) ili kuleta
ushindani katika utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha timu ya Wataalamu wa
ndani.
Timu
hiyo iliundwa na Wahandisi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi na
Wataalamu wa mazingira kutoka TBA pamoja na Mhandisi toka Wizara ya Kilimo.
Hivyo timu hiyo ilifanya upya kazi ya usanifu wa msingi, kuandaa makadirio ya
gharama za mradi, na kuandaa makabrasha ya zabuni ili kutimiza azma mbili
nilizotangulia kuzitaja hapo awali.
Matokeo
ya jumla ya kazi hiyo, yalibainisha kuwa kiasi cha fedha Dola milioni 55 kinatosheleza
ujenzi wa vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 190,000, na maghala
Tani 60,000 hivyo kufanya ongezeko la hifadhi ya Tani 50,000.
Aidha,
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unamiliki maghala ya kuhifadhi nafaka 34
yenye uwezo wa jumla ya Tani 251,000. Uwezo huu wa sasa wa maghala hautoshelezi
mahitaji ya dharula ya chakula kwa mfululizo wa miezi mitatu kwa akiba isiyo
pungua Tani 700,000, hivyo kupelekea uhitaji wa kuongeza uwezo wa uhifadhi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.