Maalim ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na wanachama wa chama hicho uliofanyika katika Hoteli ya Korini iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wanachama wake kuwa wamoja na kutoyumbishwa na upande wa Lipumba.
Amesema kuwa Lipumba ni mtu asiyekuwa mkweli, kwani yeye ndiye aliyempokea Edward Lowassa katika UKAWA lakini siku chache baadae aligeuka na kudai kuwa hakubaliani na maamuzi ya kumkaribisha katika umoja huo.
Mkutano baina ya Katibu mkuu wa chama hicho na wanachama hao ulikuwa na lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.