ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 27, 2018

WAKANDARASI MIRADI YA MAJI MAMBO SAFI.

Na Mwandishi Wetu. 

Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi Serikali kupitia wizara ya Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi ya Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu.

Mheshimiwa Aweso ameyasema hayo Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na Miradi ya DAWASCO na DAWASA.

"Wizara ya Maji inajitahidi kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo mkandarasi atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama serikali hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati" alisema Aweso Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Aweso alitembela miradi ya Maji ya Hondogo, Kibamba, Kingazi A pamoja na Mburahati.
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akiangalia bomba lililopasuka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.