Maafisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika
hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini
Wakifuatilia mafunzo ya Namna ya kutumia teknolojia ya Smart kwa njia ya
simu na kompyuta kukabiliana na Ujangili na uharibifu wa misitu
.Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha
Mweka
Maafisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika
hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini
Wakifuatilia mafunzo ya Namna ya kutumia teknolojia ya Smart kwa njia ya
simu na kompyuta kukabiliana na Ujangili na uharibifu wa misitu.
Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha
Mweka
Na Woinde Shizza,Kilimanjaro
Maafisa
Wanyamapori, maliasili, ulinzi na
uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya
serikali nchini waatanza kutumia teknolojia mpya ya kupambana na ujangili baada
ya kubaini maeneo yaliyokithiri na ujangili na uharibifu wa mazingira kwa kutumia simu na kompyuta ili kuimarisha
doria na kudhibiti ujangili.
Maafisa hao
walisema kuwa matumizi ya simu na
kompyuta zenye programu ya smart ambayo hutumiwa kuainisha maeneo hatarishi kwa
ujangili na uvunaji holela wa miti yanaweza kuwekewa alama maalum za kitaalam na kuimarisha ulinzi zaidi.
Afisa wa
chuo cha usimamizi wa wanyamapori cha
Mweka Rudolf Philemon alisema kuwa matumizi
ya teknolojia hiyo yatasaidia kukabiliana na kupunguza vitendo vya kijangili,
uvunaji haramu wa misitu na kurahisisha mbinu za kuwakamata majangili.
Rudolf
alisema kuwa kwa kutumia program hiyo ipasavyo inatarajia kupunguza vitendo vya
ujangili katika Hifadhi za taifa na mapori ya akiba ili mali asili za taifa
ziweze kuwa salama kwa manufaa ya Watanzania wote.
Mhifadhi wa
pori la akiba la Ugalla mkoani Tabora
Braka Balagaye alisema programu hiyo pia itasaidia katika kukusanya
ushahidi wa matukio mbali mbali ya majangili wanapokamatwa katika hifadhi za
taifa, mapori ya akiba na misitu ya serikali ambao unaweza kutumika mahakamani.
“Programu
hii itawarahisishia kazi askari wanaofanya doria katika hifadhi kuweza kuifanya
doria yao kimkakati na kuzaa matunda kwa kudhibiti ujangili ambao ni tatizo
sugu barani Afrika katika hifadhi nyingi” Alisema Baraka
Mkufunzi wa
programu hiyo kutoka shirika la uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori (WCS) kutoka nchini Thailand Antony Lyman alisema,
programu hiyo ikitumika ipasavyo ina uwezo mkubwa wa kutokomeza kabisa matukio
ya ujangili katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.