ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 13, 2018

WAZIRI WA MAJI AWAAGIZA WAKANDARASI WA MAJI KUMALIZA MAPEMA MIRADI HIYO

Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Katoro pamoja na Buseresere wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi kwenye Wilaya ya Chato Mkoani Geita. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo. 



Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani chato. 




Na,Joel Maduka,Geita.

Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi hiyo kwa wakati  ili  kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosekanaji  maji ambayo imeendelea kuwakabili kwa muda mrefu  .

Mhandisi  Kamwelwe ameyasema hayo  wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani  Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani  humo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo ya maji katika miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa kazi na pindi tu usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza kutekelezwa ili kumaliza kero kubwa ya maji.

Isack Saimon ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha zaidi mradi huo ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea kupata shida kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa shilingi elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza wakandarasi  wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa wananchi wa maeneo husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.


Katika  Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao wamekuwa wakuipata maji safi na salama ni  ni asilimia 41.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.