Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.Stella Manyanya(Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Msaidizi wa Mifumo wa OR TAMISEMI Baltazari Kibola wakati wa Kikao hicho kwa njia ya Mtandao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa TAMISEMI. (Picha na OR-TAMISEMI)
Mh. Mhandisi Stella Manyanya akiwa anawasiliana wakati wa kikao hicho cha siku tatu
Mkutano unaendelea na hapo wajumbe wakiwa wanasikiliza Maswali kutoka Mikoani.
Wajumbe kutokea katika Ukumbi wa Mikutano wa OR TAMISEMI, Wakiwa wanafatilia kwa karibu na kusikiliza kupitia Screen kubwa inayonekana kwa mbele maelezo na majadiliano kutoka Mikoa iliyoshiriki Kikao hicho cha siku tatu.
Manyanya:
Badilishaneni Uzoefu Katika Mageuzi ya Viwanda.
Na.
Atley Kuni – OR-TAMISEMI.
Naibu
Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mh. Mhandisi Stella Manyanya amefungua
kikao cha siku tatu mjini Dodoma kwa njia ya Mtandao (Video Conferece)
huku akiwataka wataalam katika ngazi ya
Mikoa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mwanya huo kubadilishana uzoefu
lakini pia kuibua fursa zilizopo katika maeneo yao katika uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vidogo,
vyakati na vikubwa ifikapo 2025.
Akifungua
kikao hicho Manyanya alisema, kupitia fursa ya Viongozi hao wa Mikoa na Mamlaka
za Serikali za Mitaa kukutana kwa njia ya Mtandao kutawezesha wote kuwa na
uelewa wa pamoja kuhusu mikakati ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwakupena
taarifa za kujua viwanda vilivyopo katika maeneo yao na maendeleo yake, lakini
pia kujua maeneo yaliyotengwa mahususi kwaajili ya viwanda hivyo.
“Mkutano
huu utatusaidia pia kupambanua mikakati ya kufufua viwanda vilivyokufa na namna
nzuri ya kupata wawekezaji wapya” alisema Manyanya na kuongeza kwamba lengo la mikutano hiyo nikuwa na mkakati
endelevu yakujenga uwezo kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri kuhusu masuala
ya sekta ya Viwanda, Biashara na uwekezaji.
Manyanya
amesema katika awamu ya kwanza Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA),
watatoa mafunzo juu usajili wa Biashara, Miliki Ubunifu sambamba na ujenzi wa
uchumi wa Viwanda kama falsafa ya Mh. Rais wa awamu ya tano inavyojiapambanua
kuhusu suala zima la viwanda.
Manyanya
ameongeza kuwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mh. Seleman Jafo pamoja na Waziri mwenye dhamana na Viwanda, Biashara na
uwekezaji Charles Mwijage, ni viongozi ambao kwa nafasi zao wameonesha nia ya
dhati katika kuhakikisha azma iliyowekwa na Serikali ya awamu ya Tano inatimia.
Akihitimisha
risala yake ya ufunguzi Mh. Manyanya alisema, Mikutano hiyo ni mwanzo tu, kwani
wanatarajia kuwa na chombo imara yaani kuwa na Jukwaa la Uchumi wa Viwanda kama
fursa ya kuendelea kuwezesha ujenzi na uendelezaji wa Viwanda Nchini, ambapo
wadau watajulishwa tarehe rasmi ya uzinduzi ambao utafanywa na Mh. Waziri
Mwijage.
Mkutano
huo wa siku tatu kwa njia ya mtandao ulioanza tarehe 18 na kutarajiwa
kumalizika 20 Desemba, 2017 umewakutanisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Prof. Elisante Ole Gabriel,
Makatibu Tawala wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Kilimnjaro, na Ruvuma, Mikoa
mingine ni Kigoma, Lindi, Singida na
Pwani sambamba na wataalamu wao wa Mikoa na wale wa Halmshauri.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.