Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya
Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia
Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo
Novemba 8, 2017.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya
Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi
wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisiitiza
jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na
baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es
salaam Leo Novemba 8, 2017.
Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakimlaki
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya
kuwasili kufungua Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu
cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya
Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi
wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya
Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula
wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano
lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo
Novemba 8, 2017.
Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula
wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano
lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo
Novemba 8, 2017.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya
Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Na
Mathias Canal, Dar es salaam
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
leo Novemba 8, 2017 amefungua Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na
baada ya kuvuna lenye dhima ya kujadili masuala muhimu
yanayohusiana na PHM na mchango wake katika uhakika wa chakula na kuchochea
uanzishwaji wa viwanda nchini Tanzania kwa ajili ya kupunguza upotevu, kuimarisha usalama wa chakula na
kuchochea uanzishwaji wa viwanda.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika
Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa
alisema kuwa anataraji kongamano hilo litakuwa na mjadala
muhimu kujadili masuala muhimu
yanayohusiana na Kuzuia Upotevu wa Mazao kabla na baada ya kuvunwa (PHM).
Alisema
Serikali imeweka msisitizo wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na kwa
Wabia wa Maendeleo kuwekeza katika eneo hilo la PHM.
“Serikali
kwa kuzingatia umuhimu wa sekta binafsi itahakikisha mchakato wa kutekeleza
Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza upotevu unakuwa shirikishi na unatekelezwa na
wadau kwa ufanisi”
“Nadhani
mtakubaliana na mimi kuwa hili ni tukio kubwa sana kwa Wadau wa Mpango wa kupunguza
Upotevu wa Mazao baada ya Kuvunwa (PHM) nchini tangu jitihada za kushughulikia
suala hili zianze na kwa sasa suala hili linaanza kueleweka kwa wadau wengi
tofauti na uko nyuma ambako msisitizo ulikuwa juu ya uzalishaji na tija” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema, Kulingana na takwimu zilizopo bado
kuna upotevu mkubwa wa mazao ya chakula ambao unafikia wastani wa asilimia 30 mpaka
40 kwa mazao ya nafaka na mikunde na kwa
wastani wa asilimia 50 kwa mazao ya mboga na matunda.
Alisema
ili kupunguza upotevu wa mazao ni muhimu sana na ni mkakati mzuri wa
kuihakikishia nchi usalama wa chakula na lishe. Kuwepo kwa chakula cha kutosha katika Taifa na katika ngazi ya
kaya ni msingi wa Taifa lenye uchumi imara, watu wenye afya nzuri na amani.
Alisema kuwa jitihada za
kushughulikia UPOTEVU WA MAZAO BAADA YA KUVUNWA zilianza miaka ya 1980 baada ya
kujitokeza kwa wadudu waharibifu wa mazao wajulikanao kama Dumuzi ambao walisababisha upotevu mkubwa wa mazao na kuhatarisha
uhakika wa chakula nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa Kuanzia wakati
huo mabadiliko ya kisera katika sekta ya kilimo yalianza kujitokeza kupitia
Serikali ya Tanzania hasa madiliko yanayolenga kupunguza upotevu wa mazao baada
ya kuvunwa.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa jitihada
nyingi nchini Tanzania za kupunguza upotevu wa mazao zimefanyika zikiwemo Kujenga maghala kupitia Miradi mbalimbali, Kuanzishwa
Kitengo cha Hifadhi na Usindikaji wa Mazao, chini ya Idara ya Usalama wa
Chakula na jukwaa la wadau (TPMP), Kuanzishwa kwa mashirika ya kubuni
teknolojia mbali mbali zinazohusiana na PHM kama vile SIDO, CAMARTEC, Kuigizwa
kwa masuala ya PHM kwenye Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), na Kuanzishwa
kwa miradi na juhudi mbalimbali zinazohusu PHM kama vile MIVARF, GPLP,
COWABAMA.
Mhe Mwanjelwa
alibainisha
kuwa jitihada zote hizo hazikufanikiwa vizuri kwa sababu ya kukosa mfumo mzuri
wa kuratibu kazi zote PHM zilizotekelezwa na wadau mbalimbali matokeo yake
kukajitokeza wadau kutekeleza kazi zinazofanana bila kujuana na maeneo mengine
hayakushughulikiwa kikamilifu. Hali hii ili sababisha matumizi mabaya ya
rasilima na kushindwa kuwa na mipango madhubuti ya kutekeleza shughuli za
maendeleo.
Aidha, aliwataarifa
kuwa maandalizi ya Mkakati wa Kuzuia Upotevu wa Taifa yako hatua za mwisho
ambapo Mkakati huo utaunganisha wadau wote wanaojishughulisha na kazi za
kupunguza au kuzuia upotevu wa mazao ya chakula.
“Ni Imani yangu kama mkakati huo utatekelezwa
kikamilifu upotevu wa mazao utapungua kufikia wastani wa asilimia 5 nchini
Tanzania” Alisisitiza Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa.
Ksatika hatua
nyingine Mhe Mwanjelwa alilipongeza jukwaa la wadau (TPMP) kwa kushirikiana vizuri na Wizara ya Kilimo, HELVETAS,
Swiss Inter-cooperation-Tanzania, ANSAF na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
maandalizi ya kongamano hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.