ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 20, 2017

CHALAMILA AMNADI BARAKA KIMATA KWA WANANCHI WA KATA YA KITWIRU

Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho Baraka Kimata katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
 Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgombea udiwani wa kata hiyo Baraka Kimata akiwa jukwaani kuomba kura kwa wananchi wa kata hiyo.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MAKADA mbalimbali wa chama cha mapinduzi (CCM) wamemtaka mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo pindi atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza.

Akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru mtaa wa wa Kitwiru Stand kada wa chama hicho Albert Chalamila alimtaka mgombea huyo kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha atatua kero za wananchi wa kata ya Kitwiru kwa ndio waliompa dhamana ya kuwa kiongozi katika eneo hilo.

“Leo hii tunapanda kwenye majukwaa mbalimbali kukunadi kwa kutumia akili zetu na nguvu zetu sasa ukishinda sio uanze kuwaletea kiburi wananchi wa kata hii,hapo hatuta kuwa sawa kabisa hivyo nakuomba uwaheshi na kuwatumikia vilivyo wananchi wa kata ya Kitwiru ukipewa ridhaa ya kuwaongoza” alisema Chalamila

Chalamila alisema kuwa wananchi wamekuwa wakijitokeza katika mikutano yako ya kampeni kwa lengo la kutaka kujua hoja na ahadi zako juu ya kuleta maendeleo ya kata hivyo unatakiwa kuthamini utu wao kwa kuwaletea mandeleo na kutatua changamoto zinazowakabili.

“Wananchi hawa wamekuja kwenye mkutano sio kwasasababu ya kuja kukushangaa mkutano,sio wanansimama kwa ajili kwao hawana viti,wamekuja hapa bila kupewa fedha kuja kukuona wewe bali wamekuja kukusikiliza hoja zako na kuangalia jinsi gani watapata maendeleo hivyo ni lazima uje uwatumikie vilivyo” alisema Chalamila

Chalamila akaongeza kuwa wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano ya chama cha mapinduzi mtu anayegombea kupitia chama hicho huwa anakuwa ni shupavu,Imara na muadilifu hivyo Baraka Kimata inatakuwa kuendelea kuwapa ushirikiano wananchi hawa.

“Wananchi wa Kitwiru wamejitolea kuja kwenye mikutano ya chama hiki na kuona kuwa chama kimesiamamisha mtu ambaye anasifa za kuwa kiongozi wa kuleta maendeleo kwa wananchi wake sasa ole wako uje uwageuge na uute mapembe kama walio upande wa pili” alisema Chalamila

Aidha Chalamila alimtaka Kimata kuacha kufanya kazi za wananchi kwa faida yake na kuwasahau wananchi waliokuchagua kuwa diwani wa kata hivyo chama cha mapinduzi hakiwezi kukuvumilia hata kidogo.

“Ukipewa kura na wananchi hawa unatakiwa kuwa makini sana na ukijiunga na magenge ya wahuni kwa kula rasilimali za taifa hili utalaaniwa nikwambia kweli Kimata maana saizi umebatiwa upya hivyo unatakiwa kuwa muadilifu ipasavyo”  alisema Chalamila

Chalamila alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpa kura nyingi ili awe diwani wa kata hiyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata hiyo.

“Jamani naombeni mumpe kura za ndio Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata na mumnyime kura Yule mgombea mwingine kwa kuwa Kimata yupo katika chama makini” alisema Chalamila

Kwa upande wake Kimata alisema kuwa  ameamua kugeuka kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wa kata ya kitwiru wanapata maendeleo ndio maana aliamua kugeuka.
Kimata ameendelea kuwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpigia kura nyingi siku ya tarehe ishirini na sita (26) mwezi huu ili awe diwani wa kata ya hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.