ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 8, 2017

BREAKING NEWS:- BOMU LALIPUKA NGARA NA KUUWA WANAFUNZI WATATU.

Picha kutoka maktaba.
Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu umeuwa wanafunzi watatu wilayani Ngara mkoani Kagera na kujeruhi wengine makumi kadhaa katika Shule ya Msingi Kihinga wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba wanafunzi hao walikuwa wakati wa mapumziko ya saa nne, na ndipo mlipuko huo ulipotokea na kusababisha madhara makubwa ya vifo..


Jeshi la polisi tayari lipo eneo la tukio kufuatilia na kufanya uchunguzi, na taarifa kamili zitatolewa baada ya muda mfupi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.