Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na Mbunge Joseph Kasheku Msukuma akiwa kwenye kikao hicho wakati alipokuwa akichangia hoja ya fidia kwa wananchi wa kata ya Busanda na Kaseme. |
Mjiolojia wa mgodi huo Bw Anthony Minde,akisisitiza kutokuafikia swala la kuwalipa fidia baadhi ya wananchi. |
Waziri wa Madini,Bi Angellah Kairuki akisisitiza kupereka taarifa hiyo kwenye Wizara ya ardhi kwaajili ya kutathimini kwa upya maeneo hayo. |
Baadhi ya wajumbe waliokuwepo kwenye Kikao hicho. |
PICHA NA MADUKA ONLINE.
Wizara ya
madini kwa kushirkiana na wizara ya ardhi inatarajia kufanya uhakiki upya
kwenye Mgodi wa Buckreef ili kuwalipa fidia wananchi wa kata za Busanda na
Kaseme ambao wamekuwa wakidai fidia kwa muda mrefu kwenye mgodi huo.
Hatua hiyo
imetokana na kutokuwepo kwa maelewano baina ya wabia wa Mgodi huo ambao ni
Kampuni ya Tanzam 2000 inayomiliki asilimia 55 huku asilimia 45 zikimilikiwa na shirika la madini nchini (STAMICO) waliogoma kulipa deni hilo kutokana na kutokuwa na
uhakika na madai hayo na kutokuwa na leseni.
Mjiolojia wa
mgodi huo Bw Anthony Minde alisema hakukuwepo mgogoro wowote kwani mkataba wa
uthamini ulisainiwa na mkuu wa wilaya pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita
wakati huo, hivyo suala la kulipa fidia linakuwa gumu kwa upande wao.
“Nafikiri
waliosema kwamba walikuwepo ni kwamba Afisa wa Serikali na ni wa Shinyanga,
tuliletewa baada ya kuomba kwamba hii tathmini ifanywe na mtu wa serikali
ikaidhinishwa na kusainiwa kwenye ngazi ya wilaya na mkoa kabla ya kuletwa
kwetu ili tuisome kuona kama iko sawa, Tunamshangaa Mbunge anaposema ripoti
hiyo haikusainiwa” Alisema Minde.
“Walileta
mthamini kutoka Shinyanga ambaye hakuripoti kwenye Halmashauri ya wilaya ya
Geita, ulipotokea mgogoro pale Kaseme tukaja, mlikuwa mnafanya uthamini
mnanyang’anya na marudio ya wananchi, ndo wananchi wakagoma likasimamishwa hilo
zoezi, huyo aliyekuja kurudisha kwenye ngazi ya Halmashauri ni nani
aliyeridhia? Na kama kweli mlifanya uthamini hawa asilimia mia moja wametokea
wapi?” Alisema Msukuma.
Waziri wa
Madini Bi, Angellah Kairuki amechukua uamuzi wa kupeleka madia hayo kwenye
wizara ya ardhi na kwamba atamueleza Waziri husika kurudisha wathamini wake kwa
mara nyingine ili kujiridhisha kwa kila mwananchi kama anaumiliki halali wa
eneo analoliombea fidia.
“Sasa mimi
uamuzi wangu ni kwamba, kama Serikali tutakaa tutalipeleka suala hili wizara ya
ardhi kupitia kwa waziri wa ardhi ili aelekeze wataalam wake, wathamini wake
tena kurudi kwenye jina moja baada ya jingine katika majina hayo elfu moja na
sitini na mbili kila mmoja kuweza kujiridhisha eneo lake ni lipi na kama kweli
ana umiliki nalo ili baada ya hapo sasa kama wao walikuwa wamesema hawawezi
kulipa kwa sababu hawana uhakika na orodha kamili tutakuwa tumelimliza na
wasipolipa tutakuwa tumejua nia yao sio nzuri” Alisema Kairuki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.