Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zimetoa taarifa ya pamoja zikitoa wito kwa wanasiasa na polisi nchini Kenya kuzingatia sheria katika kutatua mgogoro uliopo nchini humo.
Uchaguzi wa rais wa marudio nchini Kenya unafanyika Alhamisi wiki hii, baada ya Mahakama ya Kilele kubatilisha uchaguzi wa Agosti nane baada ya kinara wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kuwasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee.
Hivi sasa chama cha Jubilee kinasisitiza uchaguzi uendelee kama ulivyopangwa lakini muungano wa NASA unasema uchaguzi wa marudio bado haujatimiza masharti ya kuufanya uwe huru na wa haki. Odinga ametoa wito kwa wafuasi wake kususia uchaguzi huo.
Raila Odinga (kushoto) na Rais Uhuru Kenyatta |
Wapinzani wamepinga marekebisho hayo. Kenyatta amesema kuna usalama wa kutosha kwa ajili ya uchaguzi wa Alhamisi huku akitoa wito kwa wale ambao hawataki kupiga kura wasiwazuie wale wanaotaka kupiga kura.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.