Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwafundisha uzalendo kwa taifa wanafunzi wa Shule
ya Msingi Mwakichenche iliyoko wilayani Singida kama sehemu ya maadhimisho ya
kumbukumbu ya baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akikata utepe kama ishara ya kuzindua bweni la
Sekondari ya Mtinko iliyoko wilayani Singida kama sehemu ya maadhimisho ya
kumbukumbu ya baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Bweni hilo lililojengwa kwa
fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa Lipa kutokana na matokeo limepewa jina la Dkt Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akikakua ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi Mwakichenche
iliyoko wilayani Singida kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya baba wa
Taifa Hayati Mwalimu Nyerere. Vyoo hivyo vimejengwa kwa fedha kutoka serikali
kuu kupitia program ya Lipa kutokana na Matokeo.
Kiongozi wa Wanafunzi
wa Sekondari ya Ilongero Daudi William Kihanga akiishukuru serikali kuu kupitia
program ya Lipa kutokana na Matokeo kwa kuwaboreshea miundombinu ya kujifunzia.
Aidha ameshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi kwa kuwanunulia
chakula (mchele kilo 140) kama sehemu ya maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi leo amekagua miradi ya uboreshaji wa mazingira ya
kujifunzia na Kufundishia katika shule nne za Msingi na sekondari, kama sehemu
ya kumbukumbu ya Hayati baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Katika ziara yake Dkt
Nchimbi ametumia muda mwingi kuwafundisha uzalendo kwa taifa, wanafunzi wa shule
za Sekondari Ilongero na Mtinko pamoja na shule za Msingi Mtinko na
Mwakichenche zote za Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Dkt Nchimbi amesema, wanafunzi
hao watamuenzi mwalimu Nyerere na kudumisha uzalendo endapo watasoma kwa bidii
ili taifa lipate wataalamu wa kutosha katika Nyanja mbalimbali watakaoweza kusaidia
kukuza uchumi wa Tanzania.
“Mchango wa baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere kwa taifa letu ni mkubwa sana kwakuwa licha ya kutupatia
uhuru pia ametukomboa katika umasikini, ujinga na maradhi, hivyo basi nawaasa
muipende sana elimu ili na nyinyi muweze kuwa sehemu ya kulisaidia taifa”,
ameeleza Dkt Nchimbi.
Ameongeza kuwa katika
kuboresha elimu serikali ya awamu ya tano imetoa zaidi ya shilingi bilioni 1
Mkoani Singida kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kidato cha tano na sita
pamoja na kujenga miundombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa kipindi
cha mwaka 2017/2018.
“Tunapomkumbuka Mwalimu
Nyerere leo tuthamini mchango wa serikali yetu unaofanya kwa ajili ya kuboresha
sekta mbalimbali, mfano katika sekta ya elimu shilingi 1,052, 200,000 zilizotolewa
nimethibitisha zimefanya kazi nzuri, kazi kwenu walimu kufundisha kwa bidii na
wanafunzi kukazana katika kusoma kwakuwa mazingira yameboreshwa sana”,
amesisitiza Dkt Nchimbi.
Aidha Dkt Nchimbi
amewapongeza wakuu wa shule na kamati za shule hizo kwa kuchagua mafundi wazawa
ambao wametumia gharama nafuu na kujenga miradi hiyo kwa kiwango kizuri, huku akisisitiza
wananchi wasijicheleweshee maendeleo kwa kungoja wataalamu kutoka nje ya nchi
wakati mtanzania anaweza kufanya jambo hilo kwa ubora ule ule.
Naye Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Singida Rashidi Mandoa amesema serikali kuu kupitia program
ya lipa kutokana na matokeo imetoa fedha hizo kwa ajili ya shule tatu za
Sekondari na mbili za Msingi ili kuinua ubora wa elimu Wilayani hapo.
Mandoa amesema
kupitia miradi hiyo inayotekelezwa katika sekondari za Mtinko, Ilongero na
Mwanamwema Shein pamoja na shule za Msingi za Mtinko na Mwakichenche, wananchi
wameongeza imani na matumaini makubwa kwa serikali yao.
Kwa Upande wake
Kiongozi wa Wanafunzi wa Sekondari ya Ilongero Daudi William Kihanga amesema nafasi
waliyonayo katika kumuenzi baba wa Taifa ni kusoma kwa bidii kwakuwa wana imani
kuwa kila mwalimu anapenda mwanafunzi asome kwa bidii vivyo hivyo wakisoma kwa
bidii watakuwa wanamuenzi baba wa Taifa.
Kihanga ameishukuru
serikali kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia kwakuwa inawapa wanafunzi
hamasa ya kusoma kwa bidii bila kikwazo chochote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.