NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi
mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017,
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi
hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa
Wateja iliyoanza leo Oktoba 2, 2017.
“Mtakumbuka
kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja
duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili
kuboresha zaidi huduma zetu.”
Akizungumzia
mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu
ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”
Bi.
Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,
hapa
makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye
utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma
kutoka taasisi hizo washirika.
Aliwataja
washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa
Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu,
(MCB).
Alisema,
PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya
kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Miongoni
mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa
Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na
maafisa wa PSPF.
“Kwa
kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia
malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma
stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa
uchapakazi wa namna hii.” Alisema Dkt. Msengi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.