Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia mara baada ya kutangazwa matokeo ya kura walizopiga.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza jambo wakati wa Mkutano maalumu wa CCM Wilaya ya Manyoni.
Zoezi la upigaji kura katika Mkutano maalumu wa CCM Wilaya ya Manyoni.
Zoezi la upigaji kura katika Mkutano maalumu wa CCM Wilaya ya Manyoni.
Zoezi la upigaji kura katika Mkutano maalumu wa CCM Wilaya ya Manyoni.
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa CCM katika wilaya ya Manyoni Katibu wa siasa na uenezi wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mhe Mussa Sima akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu maalumu wa CCM ngazi ya Wilaya.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalumu wa CCM Wilaya ya Manyoni wakifatilia kwa makini mkutano uliiokuwa na agenda ya upigaji kura.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati) Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa CCM katika
wilaya ya Manyoni Katibu wa siasa na uenezi wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mhe Mussa Sima (Kushoto) na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Hemed Fereji wakifurahi jambo mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
Na
Mathias canal, Singida
Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha
Mapinduzi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida kwa kauli moja wametumia haki yao ya
kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za
Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.
Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya CCM eneo
la Mjini kati, Kata ya Manyoni Mjini na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi
ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za
uchaguzi wa CCM.
Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni
aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni Ndg Jumanne Ismail Makhanda kwa kupata
842, nafasi ya pili imeshikiliwa na Elia Abrahamu kwa kupata kura 199 na
Geofrey Caratta aliyeshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 29.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi katika
nafasi hiyo Mwenyekiti Jumanne Makhandi amemtaka katibu wa Chama hicho Wilaya
ya Manyoni kuandaa taarifa na mikataba ya mali zote za chama ikiwemo nyumba na
fremu za Maduka namna ya uwekekezaji ulivyo ili kubaini ubadhilifu wa mali za
chama.
Alisema kuwa ni jambo la aibu kwa viongozi
mbalimbali wa CCM hususani watendaji wa mashina, Matawi na Kata kutumia gharama
zao kueneza na kufanya shughuli za chama ilihali kuna mali nyingi za chama
zisizo eleweka namna zinavyotumika.
Aliahidi kutekeleza na kusimamia ilani ya Uchaguzi
ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 huku akiwashi wananchi kwa kauli moja
kushirikiana na Viongozi wote wa Chama na serikali hususani kumuunga mkono Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa
anayoifanya ya kuwatumikia wananchi pasina kujali maslahi yake binafsi.
Aidha, Alisema kuwa wananchama wanapaswa kuzifahamu
mali zao zitokanazo na nguvu zao katika chama ikiwa ni pamoja na kusomewa
mapato na matumizi ili kuondoa ombwe la malalamiko na sintofahamu baina ya
wananchama na uongozi wa chama.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwasihi wajumbe
wote kuwaunga mkono washindi wa nafasi zote za uongozi ndani ya CCM ili
kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika kuwatumikia.
Mhe Mtaturu alisema kuwa katika kipindi cha uchaguzi
wa ngazi ya chama na hata serikali kila mwananchi huwa na maono na mtazamo wake
kwa kiongozi amtakaye lakini pindi anapochaguliwa kiongozi mmoja ni wazi ni
vyema ikawa mwisho wa makundi hayo hivyo kuwa na mshikamano mpya katika
uwajibikaji.
Naye Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo wa CCM katika
wilaya ya Manyoni Katibu wa siasa na uenezi wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mhe Mussa Sima aliwapongeza wananchama kwa
kujitokeza kwa wingi kupiga kura, jambo alilosema wametumia vyema haki yao ya
msingi ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya CCM.
Pia alimpongeza Mwenyekiti mpya wa CCM kwa kuanza
kutema cheche za uwajibikaji katika nafasi yake huku akisema kuwa ni viongozi
wachache wenye uwezo kama wake wa kuthubutu.
Nafasi zingine zilizowaniwa ni Ujumbe wa Mkutano
Mkuu CCM Mkoa ambapo waliopata uwakilishi huo ni Leah Gervas Haule aliyepata
kura 570 na Abasi Jumanne Mayeye aliyepata kura 490.
Wengine ni wajumbe wa
mkutano mkuu CCM Taifa ambao ni Eliza Bajile kura 480, John Lwanji aliyepata
kura 417 na Neema Ukota aliyepata kura 399.
Wengine ni wajumbe wa wa Halmashauri Kuu CCM Wilaya
ambao ni Widon Mathayo aliyepata kura 610, Zabibu Shaibu kura 470, Jofrey
Farijala kura 394, Hussein Masawo 390, Lucy Mtinya 381, Abeli Razalo 361, Sauda
Masabuni 327, Wahida Magili 311, Juma Mwendi 301 na Shakira Hema aliyepata kura
289.
Nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Manyoni imenyakuliwa na Said A. Mohamed aliyemshinda mshindani wake kwa tofauti ya kura 12 ambaye ni Gervas Simion aliyepata kura 70.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.