Askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa
Pwani Laitiness Kimaro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara
baada ya kumaliza mafunzo yanayohusiana na mfumo mpya wa kuwabaini baadhi ya
madereva na wamiliki ambao wamekuwa wakitumia stika za bima feki kinyume cha
sheria na taratibu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mmoja wa askari wa kikosi cha Usalama barabarani
Mkoa wa Pwani Khalid Mohamed akifafanua
jambo mara baada ya kumaliza mafunzo ya jinsi ya mfumo mpya unaotumika katika kuwabaini
madereba hao wanaotumia bima feki.
Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani
mkoa wa Pwani wakiwa wanaendelea na zoezi la kufanya ukaguzi kwa baadhi ya
magari ambayo yanatumia stika za bima bandia.
Kaimu
kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Blasilusi Chatanda akizungumza na
baadhi ya waandishi wa habari nje ya ukumbi wa maisha plus ambapo yamefanyika
mafunzo kwa askari wa usalama barabarani juu ya mfumo mpya wa kukagua magari
ili kuweza kubaini wanaotumia bima feki kinyume na taratibu.(PICHA ZOTE NA
VICTOR MASANGU)
KATIKA kukabiliana na kupambana na
wimbi la wizi linalofanywa na baadhi ya wamiliki wa magari na
pikipiki kuamua kutumia stika za bima bandia hatimaye Mamlaka ya
usimamizi wa shughuli za bima nchini (TIRA) imeamua kutoa mafunzo kwa
askari
wa kikosi cha usalamaa barabarani Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza
Akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yamewashilikisha
maafisa wa polisi pamoja na askari wa kikosi cha usalama barabarani Kamishina
mkuu wa (TIRA) nchini Baghayo Sakwele lengo la amesema kuwa lengo la mafunzo
hayo ni kwa ajili ya kuweza kuwafundisha askari wa usalama barabarani mfumo
mpya ambao utaweza kuwasaidia kutambua na kuhakiki stika za bima ambazo ni
bandia na zinatumika kinyume kabisa na sheria na taratibu.
Kamishina huyo alibainisha
kuwa kwa sasa wameamua kushirikiana na jeshi la Polisi ili kuweza kufanya msako
wa kuweza kuwabaini wamiliki wa vyombo vya moto kutumia bima feki kitu ambacho
kinachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza kwa pato la Taifa kutokana na vitendo vya wizi ambavyo vinafanyika, na
kuongeza kuwa changamoto iliyopo ni wamiliki wengine wanafanya ujanja wa kutumia bima moja zaidi
ya magari matano.
“Sisi kama TIRA ambao ndio wenye mamlaka ya utoaji wa stika
za bima katika vyombo vya magari, tumeamua kushirikiana bega kwa began a jeshi
la polisi Mkoa wa Pwani ili kuweza kuhakikisha kuwa wale baaadhi ya wamiliki
waliokuwa na tabia ya kutumia magari yao au pikipiki kwa kutumia bima bandia
tunawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria na katika hili hatuwezi
kuwavulimilia hata kidogo,”alisema Kamishina Sakwele.
Kwa upande wake Kaimu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani Blasilusi Chatanda alisema kuwa
atalivalia njuga suala hilo la kufanya msako mkali ili kuweza kubaini mtandao
unaojihusiha na kutengeneza bima feki ili kuweza kuwathibiti wale wote ambao walikuwa wanatumia
bima bandia kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine
wenye tabia kama hiyo.
“Kama jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na
wenzetu wa Tira kwa kweli tutashirikiana
nao kwa hali na mali na kwa kuwa wameshatupatia mafunzo kuhusiana na mambo
mbali mbali ikiwemo kuwepo kwa wimbi la madereva na wamiliki wa vyombo vya moto
kuwa na tabia ya kutuia stika za bima feki tunawakamata na kuwachukulia hatua
kali za kisheria kwa hivyo vaskari wetu nina imani walilifanikisha suala hilo,”alisema
Kamanda.
Nao baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa
wa Pwani ambao wameshiriki katika
mafunzo hayo akiwemo George Peter, Laitiness Kimaro pamoja na Khalid Mohamed wamesema kuwa yatawasaidia katika kutekeleza
majukumu yao ipasavyo katika masuala mbali mbali ya kuwaelimisha madereva wa magari na pikipiki kuhusiana na
bima feki na iliyo halali.
Walisema kuwa wana imani kuwa baada ya kujifunza mafunzo hayo wataweza kufanya kazi zao za
barabarani kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa
madereva wote wa vyote vya moto ikiwemo magari pamoja na pikipiki kuhusiana na
matumizi halali ya ukataji wa bima zao pamoja na madhara ya kukata bima amabzo
ni feki.
“Kwa kweli sisi kama askari wa kikosi cha usalama barabarani
katika Mkoa wa Pwani tumefarijika sana kuuaptiwa mafunzo haya na wenzuetu wa
mamlaka ya husika, hivyo na sisi tutahakikisha elimu hii inakuwa ni chachu na
mkombozi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku pindi
tuapokuwa barabarani hivyo ni jambo ambalo kwa kweli ni faida kwetu,”walisema
askari hao.
ASKARI hao wa kikosi cha usalama
barabarani Mkoa wa Pwani
mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo walikwenda kufanya ukaguzi wa magari
barabarani kwa njia ya vitendo zaidi ambapo katika zoezi hilo
walisewe kufanikiwa kukamata
baadhi ya magari na kuyapiga faini ambayo yamekuwa bado yakiendelea
kutumia
bima feki kinyume na sheria za nchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.