ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 31, 2017

MAKOSA MAWILI ANAYOTUMIWA KUTENDA ZITTO KABWE.

HABARI MPYA:- Kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe, mkoa wa kipolisi Temeke, Dar es salaam anakoshikiliwa Zitto Kabwe

Kwamujibu wa taarifa kutoka kwenye kamati a sheria na katiba ya chama hicho, imeeleza kuwa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi.

Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:

1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.

2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

Kamati ya Sheria na Katiba
ACT Wazalendo
Oktoba 31, 2017
Dar es salaam

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.