ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 4, 2017

DC MTATURU AAGIZA WATAALAMU WA KILIMO KUWAUNGANISHA WAKULIMA NA MFUMO WA BENKI YA KILIMO

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
Wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Mipango Miji katika Halmashauri ya Itigi na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao Cha kazicha namna ya kuboresha kilimo, Ufugaji na Mipango Miji.

Na Mathias Canal, Singida

Wataalamu wa Kilimo wametakiwa kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.

Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa pamoja na wananchi kujituma katika uzalishaji wa mazao ya chakula na kilimo lakini changamoto Ni kubwa ya namna ya kuongeza ufanisi katika masoko.

Alisema kuwa endapo wakulima wataunganishwa na Benki ya Kilimo itakuwa Ni njia pekee ya kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Alisema kuwa Katika kutekeleza majukumu ya wananchi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. 

Katika kikao hicho Cha kuwakumbusha majukumu wataalamu hao Mhe Mtaturu amewataka kuandaa mpango kazi wa mazao ya Kilimo hususani mazao ya chakula na Biashara.

"Ili kuwe na kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi" 

"Tufanye hivi ili kuwa mfano Bora katika Mnyororo wa thamani ambao Ni sera ya Taifa ya viwanda kuchakata mazao ili kuondoa uuzaji wa malughafi na hivyo kuuza bidhaa" Alisema Mhe Mtaturu

Aliongeza kuwa kupitia Mnyororo wa thamani utapandisha thamani ya Mazao ya Wakulima ikiwa ni pamoja na kujiunga kwenye vyama vya Ushirika Jambo ambalo litaibua chachu ya wananchi kutilia mkazo zaidi katika kujiusisha na kilimo.

Mhe Mtaturu Alimuelekeza Katibu Tawala wa Wilaya ya Manyoni kuandaa kikao na maafisa ugani ili kukumbushana ufanisi na namna Bora ya kuendeleza Kilimo kwa wananchi kuanza kulima mazao ya kipaombele yaliyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ambayo Ni zao la Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.

Alisema pomoja na mazao ya kipaombele pia wananchi wanapaswa kuendelea kuongeza nguvu katika mazao yanayostawi kwa wingi Wilayani humo ikiwa Ni pamoja na zao la Alizeti na zao la Dengu.

Katika upande mwingine Mhe Mtaturu alishauri wataalamu wa Mifugo kutilia msisitizo Ufugaji wa kisasa (Ziro Grazing) kwa kutembelea na kupata utaalamu wa Ufugaji na mbegu Bora za ya Ng'ombe wa kisasa kwa wataalamu katika Rachi ya Taifa ya Kongwa (NARCO) na LITI iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Naye Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Chimsala Fadhili na Afisa Kilimo Umwagiliaji na ushiriki wa Halmashauri ya Itigi Ndg Renatus Mtatina walimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutangaza kufanya uzinduzi wa msimu wa Kilimo Wilaya kwani utaongeza chachu na Hamasa kwa wananchi kulima kwa wingi na tija.

Walisema kuwa miongoni mwa mambo Msingi na yenye tija katika Jamii Ni pamoja na viongozi kuwa wabunifu katika utendaji Jambo ambalo llimeonekana kwa Mkuu huyo wa Wilaya.

Uzinduzi wa msimu wa Kilimo Wilayani Manyoni utafanyika hivi karibuni ambapo utaambatana na mashindano ya Kilimo katika kila Kijiji, Kata na Tarafa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.