Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo. |
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano
mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa
uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
|
Na Fredy Mgunda,iringa.
Walimu wa halmashauri ya
manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kondomu ili kujikinga na magonjwa ya
zinaa amboya yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.
Hayo yamesemwa na katibu
tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha
walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.
Chintinka alisema kuwa
kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya
mapenzi bila kutumia kondomu.
“Jamani hapa Iringa kuna
tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu
ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa
ukimwi” alisema Chintinka
Chintinka alisema njia ya
kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana
hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya
kinga
“Naombeni tuwakinge hawa watoto
wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo
tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka
Aidha Chintinka aliwaomba
walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali
bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili
aweze kupata mgao wa pesa za lishe.
“Jamani walimu fungu la
lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili
mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni
fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka
Chintinka aliwataka
watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja
ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe
iliyotengwa na wilaya.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa
viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi
walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.
Kwa kweli mgeni rasmi
umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya
walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa
Naye katibu wa chama cha
walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa
ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda
kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.