ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 20, 2017

ASKOFU AFARIKI AKIWA SAFARINI.

 Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi limempoteza askofu wake, Castory Msemwa aliyefariki jana Alhamisi Oktoba 19,2017 saa saba mchana nchini Oman.
Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki dunia mjini Muscat akiwa safarini kwenda nchini India kwa matibabu.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imesema Askofu Msemwa alikuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili na amekuwa akipata tiba na kuendelea na utume kama kawaida.

TEC imesema Askofu Msemwa aliondoka nchini Jumatano Oktoba 18,2017 kuelekea nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.

Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu wa kuuleta nchini mwili wa marehemu Askofu Msemwa Jumapili Oktoba 22,2017 unafanyika. Amesema taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadaye.

Askofu Msemwa amezaliwa mwaka 1955 katika Kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Motola, kisha sekondari katika Seminari Kuu ya Peramiho ambako alisomea Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987. Alipata daraja ya upadri Juni 7,1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, kiongozi wa vijana parokiani jimboni Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum Pontifical College for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996.

Alipata Daraja ya Uaskofu Januari 30,2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Agosti 25,2005.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.